RAIS DK.SAMIA AWATIKISA WAKUU WA MIKOA, ATEUA WAPYA WANNE

 Mwandishi Wetu, daimatznews@gmail.com

Rais Samia Suluhu Hassan amewatikisa wakuu wa mikoa kwa kufanya uteuzi wa wakuu wa mikoa wapya wanne, akiwahamisha vituo vya kazi sita, ambapo pia ameteua Katibu Tawala mpya mmoja na kuwahamisha wengine wanne.Mbadadiliko na uhamisho huo pia umewagusa baadhi ya wakuu wa mikoa wakongwe baadhi wakiwa Adam Malima, Queen Sendiga na Martin Shigela(pichani chini).

Taarifa iliyosainiwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Bakari Machumu, leo Agosti 27,2026 ikimnukuu Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dk. Moses Kusiluka akieleza kuwa Rais Samia amemteua Alexander Mnyeti kuwa Mkuu wa Mkoa wa Geita, Jumanne Sagini kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, huku akimteua Stanslaus Nyongo kuwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani na CP. Salum Rashid Hamduni aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza kuwa Mkuu wa Mkoa huo.

Taarifa hiyo ya Ikulu imeeleza: " Martin Shigela amehamishwa kutoka Mkoa wa Geita kwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara. Said Mtanda amehamishwa kutoka Mkoa wa Mwanza kwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, akichukua nafasi ya Anamringi Macha ambaye amestaafu."

Kwa mujibu wa Ikulu, Abubakar Kunenge amehamishwa kutoka Mkoa wa Pwani kwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe akichukua nafasi ya Jabiri Omar Makame ambaye atapangiwa kazi nyingine, ambapo Beno Malisa amehamishwa kutoka Mkoa wa Mbeya  kwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora akichukua nafasi ya Paul Matiko Chacha aliyeteuliwa kuwa Katibu wa NEC-Idara ya Organaizesheni ya Chama Cha Mapinduzi(CCM).  

"..Adam Malima amehamishwa kutoka Mkoa wa Morogoro kwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi, anachukua nafasi ya Zainab Talack ambaye amestaafu, Queen Sendiga amehamishwa kutoka Mkoa wa Manyara na kuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro," imeeleza sehemu ya taarifa hiyo ya Ikulu.

Zaidi soma uteuzi wa Rais Samia hapa chini;



Post a Comment

Mpya zaidi Nzee zaidi