DK.NCHIMBI ATIMULIWA CCM, NDEJEMBI MAKAMU WA RAIS

 Mwandishi Wetu, daimatznews@gmail.com

Aliyekuwa Makamu wa Rais na Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM, Dk.Emmanuel Nchimbi(pichani kulia), amefukuzwa uanachama wa chama hicho kuanzia leo Agosti 26,2026, huku Deogratius Ndejembi (Kushoto), akitangazwa kupendekezwa kuwa Makamu wa Rais wa

Akizungumza na wanahabari usiku huu, Katibu Mkuu wa CCM, Dk. AshaRose Migiro ametoa tangazo hilo akieleza hatua ya kumfukuza Dk.Nchimbi ni uamuzi uliotokana na sababu za nidhamu na maadili, ambapo vikao vya juu vya chama vilibaini mwenendo usioridhisha wa kiongozi huyo na kuamua kumfukuza.

:Kwa kauli moja Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi imepitisha uamuzi kwamba ndugu Nchimbi afukuzwe uanachama wa Chama Cha Mapinduzi, amesema Dk. Migiro.

Kuhusu uteuzi wa Ndejembi, Katibu Mkuu wa CCM amesema uamuzi huo ni wa hatua ya awali uliopitishwa na Halmashauri Kuu ya CCM, unaosubiri hatua ya uthibitisho kwa mujibu wa Katiba.

Iwapo atathibitishwa, Ndijembi atakuwa Makamu wa Rais wa tatu kufanya kazi na Rais Samia Suluhu Hassan, akitanguliwa na Dk. Philip Mpango na Dk. Emmanuel Nchimbi, aliyejiuzulu mapema Agosti 25, 2026.

Ndejembi ameteuliwa huku akiwa nchini Marekani kuhudhuria mkutano wa kimataifa wa mawaziri kinachozindua Mpango wa Atomic Technologies Lisenced for Application at Sea(ATLAs) wa  Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomic.

Kabla ya uteuzi huo, Ndejembi ambaye ni Mbunge wa Chamwino mkoani Dodoma, amewahi kuwa Naibu Waziri, Waziri wa Ardhi na Waziri wa Nishati hadi alipoteuliwa. Alizaliwa Julai 12, 1983.

Historia yake inaonesha kuwa mwaka 2012 hadi 2014 Makamu wa Rais huyo Mteule alifanya kazi Smile Communication akiwa mkuu wa mauzo, kisha kuwa meneja mauzo, mwaka 2014 hadi 2015 alifanya kazi Kampuni ya Tigo sasa Yas kwa nafasi ya Meneja wa Kanda.

Mwaka 2016 alifanya kazi akiwa Mkuu wa Masoko wa GSm Group, ambapo mwaka 2016 hadi 2020 alikuwa Mkuu wa Wilaya.

Kuhusu elimu, historia yake inaonesha kuwa mwaka 1988 hadi 1995 alisoma elimu ya msingi katika shile iitwayo Cannon Andrea, kisha kuhitimu kidato cha nne katika Shue ya Sekondari Kigurunyembe mkoani Morogoro, mwaka 1999, Kidato cha Sita katika Merton College mwaka 2004, kisha mwaka 2009 hadi 2012 akasoma Advanced Diploma katika chuo cha Instotute of Administrative Managment.

Mwaka 2006 alihitimu shahada ya kwanza katika Uhusiano wa Kimataifa Chuo Kikuu cha  Lincoln na Shahada ya Uzamili katika Chuo Kikuu cha Colombia.


Post a Comment

Mpya zaidi Nzee zaidi