NHC ILIVYOFUNGUA FURSA ZA MAKAZI, UWEKEZAJI 88

daimatznews@gmail.com

Maonesho ya Nanenane kitaifa kwa 2026 yamekamilika jijini Dodoma, huku Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), likiacha alama ya kipekee kwa kuwafungulia fursa wananchi wanaotafuta kumiliki au kuwekeza katika sekta hiyo kwa kuitambulisha miradi mbalimbali inayotekelezwa nchini.

Katika maonesho hayo aliyotembeleawAgosti 07, 2026. Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Hamad Abdallah(pichani juu),  amesema kuwa timu ya wataalam wa shirika lake kitengo cha mauzo na wale wa huduma kwa wateja, wapo tayari wakati wowote kutoa maelezo ya kina kuhusu miradi ianayotekelezwa kama ambavyo wamekuwa wakifanya siku zote za maonesho ya Nanenane.

"Dodoma ni miongoni mwa maeneo yanayoshuhudia uwekezaji mkubwa wa NHC katika sekta ya makazi, kwa sasa Shirika linaendelea na utekelezaji wa miradi mitatu mikubwa," amesema Abdallah na kuitaja miradi hiyo kuwa ni pamoja na; 

"Mradi wa Iyumbu wenye nyumba 170, mradi unaoendelea katika eneo la Medeli, pamoja na mradi mpya wa nyumba za kisasa wa Samia Housing Scheme, ulioanza kutekelezwa mwezi huu wa Agosti.".

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu huyo wa NHC, fursa za kununua au kuingia ubia na NHC haziishii Dodoma pekee, bali shirika lake linaendelea kutekeleza na kutangaza miradi mbalimbali ya makazi na biashara katika maeneo mengine nchini.

"Miradi mingine inajumuisha Mradi wa Golden Premier Residences wa jijini Dar es Salaam, Songea Commercial Complex, Tabora Commercial Complex, Mkwakwani Plaza jijini Tanga pamoja na Iringa Commercial Complex," ameongeza Abdallah.

Amesema wananchi waliotembelea Banda la NHC msimu wa Nanenane 2026, wamepata nafasi ya kuzungumza moja kwa moja na wataalamu wa Shirika, kufahamu nyumba zilizopo sokoni, bei, namna ya kulipia, pamoja na kupata ushauri unaowawezesha kufanya uamuzi sahihi wa umiliki wa nyumba au kufanya uwekezaji.

Akizungumzia huduma za NHC, mkazi wa Dodoma, Protas Pilimini Nyoni  amesema ameridhishwa na huduma za NHC na kuwahamasisha Watanzania kutumia fursa zinazotolewa na Shirika hilo.

“NHC imekuwa ikibadilisha mandhari ya makazi nchini. Nawahamasisha Watanzania wenzangu kufika kupata huduma za Shirika hili kwa sababu lina nyumba za viwango na bei zinazowawezesha wananchi wa makundi mbalimbali kumudu umiliki wa nyumba,” amesema Nyoni.

NHC imeendelea kuwakaribisha wananchi katika ofisi zake maeneo mbalimbali nchini pamoja na kwenye mitandao ya kijamii kupata taarifa sahihi kutoka kwa wataalamu na kujionea fursa mbalimbali za makazi, biashara na uwekezaji zinazopatikana kwa kila Mtanzania.

Post a Comment

Mpya zaidi Nzee zaidi