Mwandishi Wetu, daimatznews@gmail.com
Taarifa za kujiuzulu kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Emmanuel Nchimbi zilizozagaa mitandaoni na kwenye vyombo vya habari, zimeibua hoja mbalimbali ikiwamo ya kuongezeka kwa viongozi wakuu wastaafu, lakini pia nani atakuwa mrithi wa nafasi hiyo kutoka ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Ikumbukwe kuwa tangu kuingia madarakani kwa Rais Dk. Samia, ameshafanya kazi na Makamu wa Rais wawili, wa kwanza akiwa Dk.Phillip Mpango na wa pili ni Dk. Nchimbi ambapo sasa, kiongozi mkuu huyo wa Tanzania, atalazimika kuteua mtu mwingine wa kufanya kazi naye, akiwa Makamu wa Rais wa tatu kufanya kazi naye.
Kwa mujibu wa Katiba, Rais anatakiwa kuteua Makamu wa Rais mwingine ndani ya siku 14, baada ya aliyepo kutokuwepo madarakani kwa sababu yeyote ikiwamo kujiuzulu, au kufariki dunia. Mteule huyo atalazimika kuthibitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Waraka wenye taarifa za Dk.Nchimbi kujiuzulu zilizagaa mitandaoni leo asubuhi, huku baadae Kituo cha Televisheni cha Star TV kikiripoti kuwa Dk. Nchimbi amethibitisha kujiuzulu kwake.
Taarifa ya kujiuzulu kwa Dk. Nchimbi imepokelewa kwa hisia tofauti na wananchi na wanasiasa huku baadhi wakiandika maoni yao,lakini pia kuwepo wazi kwa nafasi hiyo kunaibua WanaCCM wanaohangaika kutafuta nafasi hiyo ya usaidizi wa karibu wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.
Tayari majina ya wanasiasa mbalimbali wanaoweza kumrithi Dk. Nchimbi yameanza kutajwa, akiwamo Profesa Palamagamba Kabudi, Paul Makonda na George Simbachawene.
Taarifa ya kujiuzulu Dk.Nchimbi hii hapa chini;



Chapisha Maoni