Mwandishi Wetu, daimatznews@gmail.com
Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) na Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), wametiliana saini makubaliano, yatakayofungua ukurasa mpya kwa kuwezesha vyombo vya usafiri majini nchini kuhesabiwa.
Utiaji saini makubaliano hayo umefanyika leo, ukihusisha wakuu wa taasisi hizo NBS na TASAC.
Akiongea baada ya utiaji saini huo kukamilika, Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Amina Msengwa, amesema hatua hiyo ni muhimu kwa mustakabali ya pande hizo.
Amesema, shirikiano kati ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) na TASAC ni hatua muhimu itakayowezesha uratibu wa mfumo wa takwimu rasmi nchini.
Msingwa ameongeza kuwa hatua hiyo pia ni muhimu kwa upatikanaji wa taarifa sahihi kwa ajili ya kupanga na kutekeleza mipango ya maendeleo.
Chapisha Maoni