RAIS SAMIA ATUNUKIWA UDAKTARI WA HESHIMA URUSI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan akitunukiwa Shahada ya Udaktari wa Heshima (Honoris Causa) na Chuo Kikuu cha Urafiki wa Watu wa Urusi- (RUDN University) kutoka kwa Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Oleg Yastrebov.

Hafla hiyo iliyofanyika Chuoni hapo Moscow nchini Urusi, tarehe 04 Juni, 2026.

Rais Dk. Samia ametunukiwa Shahada hiyo ya Udaktari wa Heshima kutokana na mchango wake katika Mageuzi ya sekta ya Elimu, juhudi zake za kuimarisha Diplomasia ya Tanzania, pamoja na mchango wake katika kuimarisha hadhi ya Tanzania Kimataifa ikiwemo kupitia sekta ya Utalii.



Post a Comment

Mpya zaidi Nzee zaidi