Jaji Godfrey Isaya Mahakama ya Rushwa awa Mfawidhi Katavi

Mwandishi Wetu,daimatznews@gmail.com

Aliyekuwa Jaji wa Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Godfrey Isaya amekuwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Masijala Ndogo ya Katavi, iliyoanza kazi rasmi Machi 30 mwaka huu.

 Akizungumza katika ufunguzi wa mahakama hiyo, Jaji Is

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Sumbawanga, Fredrick Kapela Manyanda (Katikati), akimkabidhi hati ya makabidhiano Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Katavi, Godfrey  Isaya (kushoto), kuashiria kuanza  shughuli rasmi za Mahakama Kuu, Kanda ya Katavi.

aya amewasisitizia watumishi kuzingatia nidhamu katika utekelezaji majukumu yao, kuthaminiana, kupendana, ulinzi wa miundombinu, vitendea kazi vya ofisi na utendaji wa kazi mzuri kwa watumishi wote, ili kuwezesha kutoa huduma bora ya haki kwa wananchi.

Amesema Masijala hiyo mpya inatarajiwa kuwa msaada kwa wananchi wanaotoka vijijini waliokuwa wanatumia gharama kubwa kutafuta haki Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga.

"Masijala hii inasaidia wananchi wanaotoka vijijini,  kuanzia leo mashauri yote yaliyokuwa yanafunguliwa Mahakama Kuu Masijala Ndogo ya Sumbawanga yatafunguliwa Mahakama Kuu Masijala Ndogo ya Katavi.

"Wananchi walikuwa wanatoka Kijiji cha Mishamo wilayani Tanganyika wanatembea kilomita 406 kufika Mahakama Kuu Sumbawanga.

"Wananchi wanatumia siku tatu kutafuta haki, kuna wananchi wanatoka Kijiji cha Ilunde wanatembea kilomita 476 kufika Mahakama Kuu Sumbawanga, ilikuwa changamoto kubwa na wengine walikuwa wanakata tamaa,"amesema Jaji Isaya.

Amesema wanategemea kupokea mashauri mengi kutokana na uhitaji uliokuwepo.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Sumbawanga, Fredrick Kapela Machi 27 mwaka huu alikabidhi rasmi eneo jipya la kiutawala la masjala ndogo ya Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Katavi kwa Jaji Mfawidhi wa Kanda hiyo Godfrey Isaya.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Sanamu ya Bikira Maria yaonekana ndani ya Hifadhi ya Taifa Saadani

Kapteni Traole afuata huduma za afya nchini

Wawekezaji wa Oman watua nchini, wateta na NHC kuchochea mapinduzi sekta ya makazi