NHC YAELEKEZWA KUWEKEZA AFCON
Mwandishi Wetu, daimatznews@gmail.com
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk. Leonard Akwilapo(pichani), amelitaka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), kuwekeza jijini Arusha katika eneo la viwanja vitakavyotumika kwa Mashindano ya Kombe la Afrika(AFCON), mashindano yatakayofanyika mwakani 2027.
Mashindano hayo yatajumuisha uenyeji wan chi tatu ambazo ni Tanzania, Kenya na Uganda, ambapo Dk. Akwilapo amesema Serikali imeelekeza kila Wizara na taasisi za umma zifanye jambo kuwezesha ACON kuwa bora zaidi, ikiwezekana kuliko iliyofanyika Morocco na kumalizika mwaka huu 2026.
“Wizara
ya Ardhi imepima maeneo kwenye eneo la AFCON, NHC iangalie namna ya kushiriki
kwa kujenga na kuwekeza,”amesema Dk. Akwilapo na kuongeza:
“Mimi napenda mambo ya ‘Here and now’, (Hapa tulipo na sasa), natarajia NHC itafanya jambo kuwa na majengo yatakayofanikisha AFCON.”
Awali,
akimkaribisha Waziri Dk. Akwilapo kuzungumza, Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Hamad Abdallah, alisema
yupo NHC ipo tayari kusikiliza na kupokea maelekezo ya Serikali.

Maoni
Chapisha Maoni