DC ampa siku 7 Kamishna wa Ardhi

Mwandishi Wetu, daimatznews@gmail.com

MKUU wa Wilaya ya Ubungo, Albert Msando amempa siku saba Kamishna wa Ardhi Kanda ya Dar es Salaam kumaliza mgogoro wa mipaka katika hati tatu za viwanja zenye mkanganyiko alizowapa wananchi Ubungo Kibangu.

DC Msando amesema hayo alipotembelea eneo lenye mgogoro wa mipaka Ubungo Kibangu na kukutana na wenye nyumba ambao wana hati halali za kumiliki maeneo hayo.

Wananchi wanaobishania mipaka katika maeneo yao ni Edgar Rweyemamu ambaye alipata hati Novemba 18 mwaka 2023 inayoonesha eneo la njia.

Mwingine Edward Mkina ambaye hati alipata Novemba 20 mwaka 2023 ikionyesha eneo la njia na Monica Mujungu ambaye hati alipata mwaka jana ikionyesha katika eneo lake hakuna njia inayokatiza.

Akielezea Monica amesema Mahakama ilielekeza apimiwe eneo lake, eneo lilipimwa akapewa hati  akajenga ukuta katika eneo hilo.

""Nilijenga ukuta Edgar akaubomoa, hati niliyopewa hakuna njia katika eneo langu,"amesema na kuhoji kama ilikuwa halali jirani yake kubomoa ukuta.

Alipoulizwa Edgar kama wapimaji walifika katika eneo lake, alisema walifika akawapa nyaraka wakasema wanaenda kuangalia michoro kisha watarudi kutoa uamuzi .

DC Msando alisema Kamishna katoa hati tatu ya Edgar, Monica na Mkina na kwamba zote hazijafutwa.

"Natoka siku saba kutoa uamuzi wa hapa, hati ipi ifuatwe, kwa sasa eneo lisijengwe chochote mpaka ufumbuzi utakapopatikana.

"Mgogoro unasababishwa na Kamishna, katoa hati tatu, mbili zinaonyesha njia na moja haionyeshi kuwepo kwa njia katika eneo hilo.

"Naagiza Kamishna wa Ardhi Kanda ya Dar es Salaam kuonyesha kuna njia ama hakuna njia, hati iliyotolewa kimakosa ifutwe.

Eneo la mgogoro

"Baada ya siku saba itajulikana kama Kuna njia ama hakuna, hakuna mtu anayemiliki njia, ambaye hataridhishwa na uamuzi atakaofikia Kamishna wa Ardhi atafutungua kesi,"alisema Msando.

DC Msando alielekeza wanaobishania eneo la njia wabaki kwa amani wakisubiri ufumbuzi wa mgogoro wao na kwamba atakayemtukana mwenzake achukuliwe hatua.

"Monica simu unayo, tusi moja tu rwkodi kwa simu yako, Polisi kata yuko hapa, kashtaki watakuja wamkanate aliyekutukana,"alisema.

Viongozi mbali mbali wa Mtaa wa Ubungo Kibangu walihudhuria mkutano huo akiwemo Mwenyekiti wa Mtaa Hamisi Kureva na Wananchi wa nyumba za jirani.


Mwisho.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Sanamu ya Bikira Maria yaonekana ndani ya Hifadhi ya Taifa Saadani

Kapteni Traole afuata huduma za afya nchini

Wawekezaji wa Oman watua nchini, wateta na NHC kuchochea mapinduzi sekta ya makazi