Rais Samia 'atembea' katika maneno yake afanya mabadiliko Baraza la Mawaziri
-Amtema Simbachawene
- Makonda Waziri kamili wa habari
Mwandishi Wetu, daimatznews@gmail.com
Rais Samia Suluhu Hassan, amelitikisa baraza lake la mawaziri kwa kufanya mabadiliko makubwa, akitengua uteuzi wa Waziri wa Mambo ya Ndani, George Simachawene, huku akimhamisha naibu waziri wa wizara hiyo Denis Lazaro Londo kwenda kushika wadhifa kama huo Wizara ya Viwanda na Biashara.
Rais Samia Suluhu Hassan
Taarifa ya Ikulu ya leo Januari 8, 2026, imeeleza kuwa Rais Dk. Samia amemteua Patrobas Katambi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, kutoka kuwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, ambapo Mbunge wa Chaani Zanzibar, Ayoub Mohamed Mahmoud aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Kaskazini na Kusini Unguja, ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani. 
George Simbachawene
Mabadiliko hayo ya Baraza la Mawaziri yamemgusa Profesa Palamagamba Kabudi aliyeiongoza Wizara ya Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo, ambaye amehamishiwa Ofisi ya Rais Ikulu (Kazi Maalum) huku akimpandisha Paul Makonda aliyekuwa naibu wa Profesa Kabudi kurithi nafasi hiyo.
Waziri wa Mambo ya Ndani, Patrobas Katambi
Mabadiliko hayo ya Baraza la Mawaziri yamefanyika Jan 8,2026 takriban Novemba 17, 2025 hadi leo Jan 8, 2026 takriban mwezi mmoja na siku 21 tangu kuundwa baraza la kwanza la kipindi cha pili cha Serikali ya Awamu ya Sita.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Ayoub Mohamed Mahmoud
Hata hivyo, hatua hiyo ya Rais inaweza kuelezwa ametembea kwenye maneno yake.
Ikumbukwe kuwa akizungumza mara baada ya kuapisha mawaziri aliowateua, Novemba 18, 2025 Ikulu Chamwino jijini Dodoma, Rais Samia alisema haoni taabu kubaili mawaziri.
Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo, Paul Makonda
Mbali na uteuzi na kutengua uwaziri, Rais Samia pia amefanya uteuzi wa nafasi mbalimbali ikiwemo mabalozi.
TaSoma taarifa kamili ya Ikulu iliyosainiwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Bakari Machumu, hapa chini;


Maoni
Chapisha Maoni