Ndoto mabasi ya umeme Z'bar yatimia

 Ndoto imetimia, ndivyo unavyoweza kueleza, baada ya awamu ya kwanza ya mabasi ya Mradi wa Mabasi Yanayotumia Umeme (Zan Bus) kuwasili katika Bandari ya Malindi, Zanzibar.


Kuwasil kwa mabasi hayo ya mradi unaoratibiwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) na utasimamiwa na Kampuni ya Usafirishaji ya Unitrans kutoka Afrika Kusini ni kutimia kwa ndoto ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), kupunguza taabu ya usafiri kwa wananchi.

Mabasi hayo 10 yamawasili Januari 26, 2026 na kuelekea katika maegesho ya Stendi Mpya ya Kijangwani, Mkoa wa Mjini Magharibi yakitarajiwa kuanza kutoa huduma rasmi za usafiri wa abiria mwezi ujao Februari.

Hatua hiyo pia inalenga kupunguza msongamano wa magari barabarani pamoja na kuboresha usafiri rafiki wa mazingira Zanzibar.

Mradi huo wa Zan Bus unaotarajiwa kuendelea kutekelezwa hatua kwa hatua ni sehemu ya juhudi za Serikali ya Awamu ya Nane ya uongozi wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Sanamu ya Bikira Maria yaonekana ndani ya Hifadhi ya Taifa Saadani

Kapteni Traole afuata huduma za afya nchini

Wawekezaji wa Oman watua nchini, wateta na NHC kuchochea mapinduzi sekta ya makazi