Spika Zungu aapishwa, aanza kazi bungeni
Mwandishi Wetu, daimatznews@gmail.com
Mgombea uspika wa Bunge wa CCM, Mussa Azzan Zungu (Pichani chini), ameanza kutekeleza wajibu wake mpya akiwa Spika wa Bunge la 13 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, baada ya kuchaguliwa na na wabunge na kuapishwa leo Novemba 11,2025 bungeni jijini Dodoma.
Zungu ambaye ni Mbunge wa Ilala, Dar es Salaam (CCM), ameanza kazi hiyo, baada ya kushinda kwa kupata kura 378 kati ya kura halali 380 kutoka kwa wabunge 383 waliopiga kura.
Jana, Ofisi ya Bunge ilipitisha wagombea sita kuwania uspika wa Bunge la 13 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Zungu aliyekuwa Naibu Spika kwenye Bunge lililopita ambalo Spika wake alikuwa Dk. Tulia Ackson, ambapo wagombea wengine wa nafasi ya Spika wa Bunge walikuwa ni Veronica Tyea wa chama cha National Reconstruction for Democracy (NRA), Anna Mgaya wa National Leagur for Democracy(NLD) na Chrisant Nyakitita wa chama cha Democratic Party (PD).
Wengine ni Ndonge Said Ndonge wa chama cha Alliance for Africa Farms Party (AAFP) na Alfred Yango wa chama cha Alliance for Democratic Change (ADC).

Maoni
Chapisha Maoni