Sita wapitishwa 'kuvaa viatu' vya Dk. Tulia uspika

 Mwandishi Wetu, daimatznews@gmail.com

Wagombea sita wameptishwa na Ofisi ya Bunge kuwania kuwa Spika wa Bunge la 13 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, huku mgombea wa CCM, Mussa Azzan Zungu (Pichani chini), akionekana kuchomoza zaidi 'kuvaa viatu vya uspika' .

Zungu aliyekuwa Naibu Spika kwenye Bunge lililopita ambalo Spika wake alikuwa Dk. Tulia Ackson, ana nafasi kubwa ya kutwaa uspika wa Bunge kutokana na ukweli kwamba, chama anachokiwakilisha (CCM), kina idadi kubwa ya wapiga kura katika uchaguzi wa Spika, ambao ni wabunge, huku wagombea wengine vyama vyao vikiwa havina wabunge.

Mbali na Zungu wa CCM, wagombea wengine wa nafasi ya Spika wa Bunge ni Veronica Tyea wa chama cha National Reconstruction for Democracy (NRA), Anna Mgaya wa National Leagur for Democracy(NLD) na Chrisant Nyakitita wa chama cha Democratic Party (PD).

Wengine ni Ndonge Said Ndonge wa chama cha Alliance for Africa Farms Party (AAFP) na Alfred Yango wa chama cha Alliance for Democratic Change (ADC).

Taarifa kamili ya Bunge kuhusu Uchaguzi wa Spika soma hapa chini;...




Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Sanamu ya Bikira Maria yaonekana ndani ya Hifadhi ya Taifa Saadani

Kapteni Traole afuata huduma za afya nchini

Wawekezaji wa Oman watua nchini, wateta na NHC kuchochea mapinduzi sekta ya makazi