Jicho la Rais lamwona Dk. Bashiru, Dk. Gwajima ubunge

-Yumo aliyekuwa Mkurugenzi wa PSSSF

Mwandishi Wetu, daimatznews@gmail.com

Jicho la Rais Dk. Samia Suluhu Hassan limemwona Katibu Mkuu wa zamani wa CCM, Dk. Bashiru Ally. Ndivyo unavyoweza kusema baada ya Kada huyo wa CCM kuwemo katika uteuzi wa pili wa Rais Samia tangu alipoapishwa kuiongoza Tanzania kwa miaka mitano ijayo, wiki moja iliyopita. Uteuzi wa kwanza wa Rais Samia tangu alipoapishwa Novemba 4,2025 ni wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari.

Dk. Bashiru akizungumza katika moja ya mikutano ya CCM

Uteuzi wa Dk. Bashiru na wengine watano  kuwa wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, umekuja siku moja kabla kuanza kwa Bunge la 13 kesho, unaoweza kubeba mitazamo tofauti miongoni mwa Watanzania hasa wafuatiliaji wa masula ya kisiasa na mustakabali wa taifa, hasa kipindi hiki baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, ulioshuhudia machafuko kwenye baadhi ya maeneo nchini. 

Mbali na Dk. Bashiru, wengine walioteuliwa ni Dk. Dorothy Gwajima, aliyekuwa Waziri katika Serikali wa Rais Dk. Samia 2021-2025, yumo pia Balozi Mahmoud Thabit Kombo, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Abdullah Ali Mwinyi, Balozi Khamis Mussa Omar na Dk. Rhimo Simeon Nyansaho aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa Watumishi wa Umma(PSSSF). 


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Sanamu ya Bikira Maria yaonekana ndani ya Hifadhi ya Taifa Saadani

Kapteni Traole afuata huduma za afya nchini

Wawekezaji wa Oman watua nchini, wateta na NHC kuchochea mapinduzi sekta ya makazi