Msimu wa Korosho waanza, tani 700,000 kuvunwa, kuuzwa

 -Mkurugenzi CBT asema kampuni 45 zimejiandikisha

Mwandishi Wetu, daimatznews@gmail.com

Msimu mpya wa korosho kwa mwaka huu wa 2025/2026 unazinduliwa leo Novemba 7, 2025 nchini huku taifa likitarajia kuvuna tani 700,000 za korosho. 

Korosho ghafi

Kiwango hiko ni kikubwa kwa kulinganisha na  lengo la mwaka jana, la kuvuna tani 500,000 na kufanikiwa kuvuka lengo hilo kwa kuvuna tani 528,000.

Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Korosho nchini(CBT), Francis Alfred amesema kuwa tayari zaidi ya kampuni zaidi ya 45 zimejiandikisha kununua korosho katika minada itakayoendeshwa maeneo mbali mbali yanayozalisha korosho hususan mikoa ya kusini. 

Mkoani Mtwara mnada wa kwanza wa uzinduzi utafanyika katika Kijiji cha Mchichira wilayani Tandahimba, ambao utaendeshwa na Chama Kikuu cha Ushirika cha Tandahimba, Newala,  (TANECU).

Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho Francis Alfred 

Meneja Mkuu wa TANECU, Mohamed Mwinguku amesema wanatarajia kukusanya tani 120,000 za korosho huku Chama Kikuu cha Ushirika kinachosimamia Wilaya za Mtwara, Masasi na Nanyumbu, (MAMCU), kikitarajiwa kuanza mnada wake wa kwanza katika Halmashauri ya Wilaya ya Nanyamba Novemba 10, 2025.

Meneja Mkuu wa MAMCU, Biadia Matipa amesema chama hicho kinatarajia kukusanya tani 130,000 kutoka kwa wakulima wake kwa msimu huu.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Sanamu ya Bikira Maria yaonekana ndani ya Hifadhi ya Taifa Saadani

Kapteni Traole afuata huduma za afya nchini

Wawekezaji wa Oman watua nchini, wateta na NHC kuchochea mapinduzi sekta ya makazi