Fahamu matokeo ya std VII ya mwanao 2025
-Necta yaweka hadharani matokeo
-Ufaulu waongezeka, ubora wapanda
Mwandishi Wetu, Daimatznews@gmail.com
Baraza la Mitihani la Taifa(Necta), leo Novemba 5,2025 limetangaza matokeo ya Mtihani wa Darasa la Saba nchini, uliofanyika Septemba mwaka huu.
Katibu Mtendaji wa Necta, Profesa Said Ally Mohamed ametangaza matokeo hayo leo, kufuatia mtihani huo uliofanyika kuanzia Septemba 10, 2025.
Kwa mujibu wa Profesa Mohamed, watahiniwa 1,172,279 wavulana wakiwa 535,138 na wasichana 637,141, idadi hiyo ikiwa asilimia 54.35 wasichana na wavulana asilimia 45.65 walifanya mtihani, huku akibainisha ongezeko la ufaulu kwa asilimia o.93.
"Jumla ya watahiniwa 1,146,164 waliofanya mtihani, wamefaulu kwa kupata daraja la juu A,B na C," amesema Profesa Mohamed na kuongeza;
"Ubora wa ufaulu pia umepanda na kuimarika ukiwa na ongezeko la asilimia 1.07 kutoka asilimia 35.83 mwaka 2024 hadi asilimia 36.90 mwaka huu ambapo watahiniwa 422,923 wamepata daraja A na B."
Kwa mujibu wa Necta, mwaka 2024, ufaulu ulikuwa asilimia 81.21.
Kwa matokeo ya mwanao fuata kiunganishi hapa chini;
https://matokeo.necta.go.tz/results/2025/psle/results/shl_ps0204016.htm

Maoni
Chapisha Maoni