BREAKING NEWS;Dk.Tulia aachana na uspika

 Mwandishi wetu, daimatznews@gmail.com 

Spika wa Bunge wa lililomaliza muda wake, ambaye pia alikuwa akigombea tena nafasi hiyi, Dk. Tulia Ackson, (Pichani chini), ametangaza kuachana na nafasi akijitoa kuiwania.

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania(TEF), Deodatus Balile amethibitisha uamuzi huo wa Dk.Tulia akieleza; "Nimezungumza na Mhe. Spika wa Bunge Tulia Ackson, amenithibitishia kuwa amejiondoa katika mchakato wa kuwania Uspika ndani ya CCM. Ameniambia niwajulishe Wahariri wote."

Hata hivyo, Balile amesema katika mazungumzo yao, Dk. Tulia hakutoa sababu za uamuzi huo.

"Hakuniambia sababu," amesema Balile.

Dk. Tulia alichukua fomu ya kuwania tena nafasi hiyo ndani ya CCM, huku Naibu Spika, Mussa Azan Zungu naye, akiwa amechukua fomu kuwania uspika.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Sanamu ya Bikira Maria yaonekana ndani ya Hifadhi ya Taifa Saadani

Kapteni Traole afuata huduma za afya nchini

Wawekezaji wa Oman watua nchini, wateta na NHC kuchochea mapinduzi sekta ya makazi