- Yasema haibagui ipo kwa ajili ya Watanzania wote
- Majengo yasiwaogopeshe
Mwandishi Wetu, daimatznews@gmail.com
Uongozi wa Hospitali ya Shifaa ya Dar es Salaam umewashauri wananchi wenye changamoto za kiafya na maradhi mbalimbali walio na bima ya afya ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), kufika hospitalini hapo ili wapatiwa huduma na kuacha fikra kwamba hospitali hiyo haipokei wagonjwa wanaotumia bima ya NHIF.
![]() |
Sehemu ya Jengo la Hospitali ya Shifaa iliyopo Kinondoni, Dar es Salaam linavyoonekana. |
Akizungumza ofisini kwake jijini Dar es Salaam mwishoni mwa
wiki iliyopita, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo, Bashir Haroun ametoa ushauri
huo akieleza kuwa kumekuwepo dhana potofu kwamba Hospitali ya Shifaa haipokei
wagonjwa wanaotumia Bima ya Afya ya NHIF, jambo ambalo amesema halina ukweli.
Hospitali hiyo ya kisasa ya Shirika la Shifaa Pan African
Hospitals Limited chini ya Kundi la Makampuni ya Oil Com, iliyoanza kazi miaka
miwili iliyopita, ipo maeneo ya Kinondoni, Barabara ya Msese, ikiwa na kauli
mbiu ya kuboresha huduma za afya nchini, uwekezaji wake ukigharimu Dola za
Marekani milioni 60, takriban Shilingi bilioni 162.
“Hospitali ya Shifaa inatoa huduma kwa wote bila kubagua
hali ya maisha, tunapokea na kuwatibu pia wananchi wanaotumia Bima ya Afya ya
NHIF, tofauti na mtazamo wa baadhi ya watu, wenye lengo la kuwakosesha wananchi
huduma bora na za kisasa za hospitali yetu.Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Shifaa, Bashir Haroon
Hata wale wanaosita kuja kwa kuogopeshwa na mazingira bora ya jengo la hospitali, wasiogope kuja hilo ni moja ya lengo letu kutoa huduma bora za afya katika mazingira bora,” amesema Bashir.
Ameongeza: “Hospitali ya Shifaa imejengwa kuunga mkono
juhudi za Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan za kutoa huduma bora
za afya kwa wananchi wote bila ubaguzi.
Hapa tunapokea wagonjwa wenye bima ya afya ikiwamo Bima ya
Afya ya NHIF, waje tu tutawapa hudumia bora za kisasa bila kikwazo, pia tunapokea
na kuwahudumia wanaolipa pesa taslimu.”
Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo Mtendaji, ujenzi wa Shifaa
Hospitali umezingatia mambo matatu muhimu ambayo ni pamoja na miundombinu bora
ya kisasa, vifaa tiba bora na vya kisasa ikiwamo vipimo na watoa huduma wenye
viwango bora vya taaluma.Moja ya maeneo ya kuhudumia wananchi katika Hospitali ya Shifaa, Dar es Salaam.
Bashir amesisitiza; “Tupo kwa ajili ya Watanzania, tunaunga
mkono juhudi za Serikali kutoa huduma bora za afya. Hapa hatubagui bima ya
afya, pia tuna kitengo cha ustawi wa jamii. Muhimu Watanzania wapate huduma
bora za afya.”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni