Kairuki: Mkinichagua Kibamba itabamba
Mgombea Ubunge Jimbo la Kibamba kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM), Angela Kairuki (Pichani chini kushoto), amezindua kampeni za kuwania kiti hicho leo Septemba 7,2025, akisema kuwa iwapo wananchi wa jimbo hilo watamchagua kuwa mbunge wao katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29,2025 basi 'Kibamba Itabamba.'
Kairuki ametoa kauli hiyo kwenye mkutano wake wa kwanza wa kampeni eneo la Mbezi Stendi jimboni humo mkoani Dar es Salaam ambapo amesema anazijua changamoto za jimbo hilo na matarajio yao, kwa kuwa yeye ni 'mtoto' wa Kibamba na kuwaahidi wananchi kwamba atawatatulia changamoto zote zilizopo jimboni humo."...Mimi ni mtoto wa Kibamba, nimekulia Kibamba, nimeyaishi maisha ya Kibamba, nimeyaishi mafanikio ya Kibamba, lakini pia changamoto za Kibamba, najua matamanio, nayajua pia matamanio ya wana Kiamba.
Niwahakikishie, nimedhamiria kuunganisha nguvu zangu na zenu, ili kupata majawabu ya changamoto za Kibamba. Niwahakikishie, endapo mtamchagua Dk. Samia Suluhu Hassan kwa nafasi ya urais, endapo mtanichagua mimi kuwa mbunge wenu na madiwani wote wa CCM, Kibamba itabamba, itakuwa haina mbambamba" amesema Kairuki na kuongeza:
"Mimi ni mtoto wenu, ... mtumishi wenu na mgombea wenu wa nafasi ya ubunge kwa tiketi CCM."
Maoni
Chapisha Maoni