Ada Cottrell yawasaidia watoto wenye mahitaji Zanzibar
Mwandishi Wetu, Zanzibar
Taasisi ya Ada Cottrell Foundation kwa kushirikiana na Taasisi ya Labayka Development Foundation (LDF), imetoa msaada kwa watoto wanaoishi kwenye mazingila magumu ili kuwawezesha kujikimu kwa mahitaji yao.
Msaada
huo umetolewa kwa Watoto hao walio katika Kata ya Nungwi, Kijiji cha Nungwi,
Wilaya ya Kaskazini A na Mkoa wa Kaskazini Unguja, visiwani Zanzibar.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukabidhi
msaada huo, Mkurungezi Muwakilishi wa taasisi ya Ada Cottrell Foundation, Shedrack Gabriel Albert amesema hatua
hiyo ni mwendelezo wa utaratibu unaofanywa kila mwaka na taasisi hiyo, ikiwa ni
kumbukizi ya Marehemu Robert Cottrell, raia ya Marekani kila ifikapo Agosti kwa kuwa ndio mwezi
aliofariki.
Robart ambaye alikua ni Daktari nchini Marekani alifariki
dunia Agosti 2018 kwa ugonjwa wa saratani na ameacha mke, Joyce Cottrell na mtoto wa
kike, Ada Cottrell ambaye ndiye msimamizi wa taasisi ya Ada Cottrell Foundation
ya Marekani na tawi lake kwa sasa lipo nchini Tanzania.
Hata hivyo, Shedrack amesema pamoja na msaada ukliotolewa
na taasisi yake, visiwa vya Unguja bado vinakabiliwa na changamoto ya watoto wanaoishi
kwenye mazingira magumu, hivyo bado wanahitaji msaada zaidi.
Akizungumza baada ya Watoto hao kukabidhiwa msaada huo, mwenyeji wa Taasisi ya Ada Cottrell, Khamis Juma Mtwana kutoka taasisi ya Labayka Development Foundation(LDF), iliyopo Nungwi ameahidi kushirikiana vyema kuhakikisha wanapunguza tatizo la watoto wenye uhitaji mjini humo.
Pamoja na ugawaji wa mahitaji hayo pia ilifanyika dua
maalum ya kumuombea Robart Cottrell ikiwa sehemu ya kumbukumbu yake,
iliyoongozwa na Sheikh Apite Haji Ali,
Jinala.
Maoni
Chapisha Maoni