NHC YAKABIDHI MSAADA KWA WATU WENYE ULEMAVU UBUNGO
Mwandishi Wetu, daimatznews@gmail.com Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), kupitia kwa Ofisa wake Mkuu wa Habari, Yahya Charahani, limekabidhi msaada wa vifaa vya kusaidia watu wenye ulemavu kwa Chama cha Watu Wenye Ulemavu katika Manispaa ya Ubungo, jijini Dar es Salaam. Ofisa Mkuu wa Habari wa Shirika la Nyumba Tanzania (NHC), Yahya Charahani, akikabidhi msaada wa vifaa vya kusaidia watu wenye ulemavu kwa Chama cha Watu Wenye Ulemavu katika Manispaa ya Ubungo, jijini Dar es Salaam, leo Septemba 18,2025. Msaada huo umejumuisha magongo ya kutembelea (crutches), baiskeli za walemavu, na vifaa vingine vya kusaidia watu wenye uhitaji maalum kushiriki kikamilifu kwenye shughuli za kijamii na kiuchumi. Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano, Charahani alisema: "Tumefika hapa leo kwa niaba ya Shirika la Nyumba la Taifa kuonyesha mshikamano wetu na watu wenye ulemavu. Tunatambua changamoto wanazopitia, na msaada huu ni sehemu ndogo ya mchango wetu kwa jamii ambayo sisi pia ni sehemu ya...