Serikali sasa kusaini muongozo mshahara KCC kwa Sekta Binafsi
Mwandishi Wetu, daimatznews@gmail.com
SERIKALI imesema hivi karibuni inatarajia kusaini muongozo wa Kima Cha Chini Cha Mshahara (KCC) kwa TaasisiI Minafsi zinazofanywa kazi nchini, ili kuwa sheria.
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Ajira Vijana na Wenye Ulemavu, Ridhiwan Kikwete.
Imesema katika miongozo huo inatarajia kuainisha viwango vipya vya mshahara ambapo wafanyakazi Wa sekta binafsi watakuwa wanalipwa.
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Ajira Vijana na Wenye Ulemavu, Ridhiwan Kikwete amesema hayo jijini Arusha katika uzinduzi wa Jengo la Biashara Shirikisho la Vyama Vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), lililoko mkabala na soko kuu, jijini humo.
Kuhusu miongozo huo Ridhiwan amesema tayari mazungumzo yameshafanyika baina ya wadau ambao ni taasisi binafsi na wasimamizi wa sera, pamoja na uongozi wa timu Ya Wizara uliopewa jukumu la kusimamia marekebisho hayo.
Amesema kikao kilichobakia ni cha mashauri ,ambapo watashauriana na wenzao juu ya viwango vilivyowekwa na baada ya hapo mapema mwezi ujao huenda wakasaini marekebisho hayo.
“Nawaambia wafanyakazi kuwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan anathamini sana maslahi yenu,” amesema Ridhiwan na kuongeza: "Serikali Itaendelea kuboresha Sheria za Wafanyakazi Ili ziendane na mahitaji yao."
Kwa mujibu wa Ridhiwan, Serikali itaendelea kushirikiana na wafanyakazi bega kwa bega katika kutekeleza mikakati ya kuongeza ajira, kulinda haki za wafanyakazi, na kuimarisha mifumo ya utatuzi wa migogoro kwa njia ya mazungumzo.



Maoni
Chapisha Maoni