Waziri Jafo kufungua maonesho ya ‘Tanzania Dental Expo’ Dar kesho

Na Mwandishi Wetu, daimatznews@gmail.com

Waziri wa Viwanda na Biashara,Dk.Selemani Jafo, anarajiwa kufungua maonesho ya huduma ya kinywa na meno  ‘Tanzania Dental Expo’ yatakayofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam kwa siku mbili kuanzia kesho Ijumaa Mei 30,2025.

Mkurugenzi wa Tanzania Dental Expo Dk. Ambege Jack Mwakatobe.

Maonesho hayo ya kihistoria yaliyoandaliwa kwa ushirikiano kati ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)  na Tanzania Dental Expo, pamoja na mambo mengine yawaleta pamoja wataalamu wa afya ya kinywa na meno kutoka ndani na nje ya Tanzania na maandalizi yamekamilika.

"Kutakuwa na hudima  ya vipimo na ushauri bure wa kitaalamu kwa watu wenye matatizo ya afya ya kinywa na meno kutoka kwa wataalamu wabobevu.Lakini pia, kutakuwa na maonesho ya vifaa tiba vya kisasa vinavyotumika katika kutoa huduma na kuwawezesha watoa huduma wa ndani na nje kubadilishana uzoefu katika kuboresha sekta hiyo," amesema Mkurugenzi wa Tanzania Dental Expo Dk. Ambege Jack Mwakatobe.

Dk. Mwakatobe amesema  maonesho hayo yatasaidia kuonyesha pia maendeleo ya tasnia kinywa na meno hapa nchini, ambapo ameaomba wadau mbalimnali na wananchi kujitokeza kwa wingi.

 “Tunategemea wataalamu kutoka mabara tofauti ikiwemo Ulaya, Asia na Marekani, kuja na teknolojia mbalimbali za kisasa zinazotumika katika kutoa huduma za kisasa za afya ya kinywa na meno,” amesema Dk. Mwakatobe.

Amebainisha kuwa maonesho hayo ni fursa kwa wataalamu kutoka hospitali na vituo mbalimbali vya afya ya kinywa na meno nchini kupewa mafunzo yanayohusteknolojia ya kisasa inayotumika katika kutoka hudumahizo.

Kwa mujibu wa Dk. Mwakatobe, takribani watu bilioni 3.5 duniani wakiwemo Watanzania wana changamoto mbalimbali zinazohusiana na afya ya kinywa na meno.

“Hivyo, maonyesho na upimaji huo itakuwa ni fursa pekee kwa Watanzania wenye changamoto ya afya ya kinywa na meno kupewa bure huduma ya ushauri na vipimo itakayotolewa wakati wa maonesho hayo na wataalamu waliobobea kwa kutumia vifaa vya kisasa,” amesema Dk. Mwakatobe ambaye ni mwakilishi wa Tanzania katika Shirikisho la Afya ya Kinywa na Meno Duniani (FDI).

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Maonesho hayo, Dk. Baraka Nzobo amesema kuwa maonesho hayo ni muhimu kwa Watanzania na nchi jirani, ambapo wataalamu mbalimbali watakusanyika kwa  ajili ya sekta hiyo muhimu ya afya ya kinywa ma meno kwa binadamu.

“ Maonesho haya ni fursa kubwa kwa nchi yetu kwani ni kwa mala ya kwanza kufanyika nchini ambapo yataleta wageni wa kimataifa wanaoshughulika na kutoa huduma na matumizi ya vifaa tiba vya kisasa vinavyotumika katika nchi zilizoendelea duniani,” amesema Dk. Nzobo na kufafanua:.

“Kupitia maonesho haya, tunategemea mageuzi makubwa kwa watoa huduma wa sekta ya afya ya kinywa na meno hapa nchini kwa kujifunza teknolojia inayotumika katika kutoa huduma na kuongeza weledi katika kazi zao .” 

Aidha, Dk. Nzobo meiwataka wadau mbalimbali zikiwemo taasisi za kibenki na Bima za Afya kujitokeza kushiriki katika maonesho hayo kwani yataenda kubainisha maeneo mahususi ambayo yatawaweza kuunganisha taasisi hizi na zile za kinywa na meno kuweza kufanya kazi kwa pamoja.

Naye Dk. Leonora Assevi amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi na kushiriki maonesho hayo na kujifunza namna ya kutunza afya zao za kinywa na meno na kukabiliana na changamoto mbalimbali ikiwemo harufu mbaya ya kinywa, matumizi sahihi ya kupiga mswaki.


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Sanamu ya Bikira Maria yaonekana ndani ya Hifadhi ya Taifa Saadani

Kapteni Traole afuata huduma za afya nchini

Wawekezaji wa Oman watua nchini, wateta na NHC kuchochea mapinduzi sekta ya makazi