Rais ampeleka Ngorongoro Badru wa PSSSF, Dk. Doriye mhh..
-Dk.Nyansaho bosi mpya PSSSF
Mwandishi Wetu,daimatznews@gmail.com
Rais Samia Suluhu
Hassan,pichani chini ametengua uteuzi wa Dk. Elirehema Joshua Doriye aliyekuwa Kamishna wa
Uhifadhi katika Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro (NCAA), huku akimteua Abdul-Razak
Badru kushika nafasi hiyo.
Kabla ya uteuzi huo,Badru alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), ambapo Rais Samia amemteua Dk. Rhimo Simeon Nyansaho kuwa Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, awali alikuwa Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara katika Benki ya Azania.
Dk. Nyansaho Abul- Razak Badru
Kwa mujibu wa taarifa
iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dk. Moses Kusiluka, kupitia
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais – Ikulu, Rais amefanya mabadiliko hayo ya
uongozi kwa lengo la kuboresha utendaji kazi na kuimarisha usimamizi wa
rasilimali katika taasisi hizo muhimu za Serikali.
Maoni
Chapisha Maoni