Wafanyabiashara Kariakoo wapewa siku 14 kufungua barabara
Na Hellen NGOROMERA, daimatznews@gmail,com
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila ametoa wiki mbili kwa wafanyabiashara ndogo ndogo katika Soko la Kariakoo, kufungua barabara walizofunga kwa kuweka biashara zao.Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila
Chalamila amesema hayo Mei 28, 2025 jijini Dar es Salaam alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu maendeleo ya ujenzi wa Soko la Kariakoo.
“Wafanyabiashara waliofunga barabara kwa kuweka meza na kuzuia uingiaji wa magari makubwa kwa ajili ya kuingiza biashara mbalimbali ndani ya soko.
“Natoa rai kwao uongozi wa wafanyabiashara ndogo ndogo waanze kufungua biashara hizo ili mwisho wa siku soko litakapofunguliwa kusiwe na hitilafu ya aina yoyote kuhusu kuingia au kutoka kwa kutumia njia za sokoni hapo,” amesema RC Chalamila akiongeza:
"Wafanyabiashara hao wataniuliza watakwenda wapi? Katika soko jipya linalojengwa, wameratibu namna ya wafanyabiashara wote kukaa wakiwemo wafanyabishara ndogo ndogo kwa kuweka viduka vidogo vidogo.”.
“Uongozi wa Machinga katika eneo la Kariakoo ili waweze kukaa na wafanyabishara ndogo ndogo, wawaeleze kuhusu azma ya Serikali na namna ya kufungua njia ili kila mmoja abebe mzigo huu kwa kufungua njia ili mwisho lisije kuwa soko lisilo na tija kwa uwekezaji mkubwa ambao tumeshafanya.” amesema Chalamila.
Kuhusu ulinzi usalama, RC Chalamila amesema soko hilo litafungwa kamera zitakazosaidia kubaini mienendo ya watu wazuri na wabaya kama njia ya kuondoa au kupunguza uhalifu.
“Kwa kuwa ni soko la Kimataifa na la kisasa lazima lifungwe mifumo ya kamera itakayosaidia kubaini mienendo ya wale wote wazuri na wabaya watakaokusudia au kuwa na wizi ama majaribio ya aina yoyote katika eneo hilo.
“Ikumbukwe kuwa kutakuwa na mabenki na wataoa huduma, kutakuwa na wafanyabiashara wakubwa watakaokuwa wakifanya biashara za kuingia na kutoka katika eneo hilo,” amesema Chalamila.
Pamoja na mambo mengine, amesema hali hiyo itasaidia kuwapa urahisi wafanyabiashara kutoka katika maeneo ya ndani na nje ya nchi kupata huduma kwa urahisi
Maoni
Chapisha Maoni