DC Ubungo sasa Mkurugenzi mpya Tanesco


Mwandishi Wetu,daimatzanews@gmail.com
Rais Samia Suluhu Hassan, amemteua Mkuu wa Wilaya ya Ubungo,Dar es Salaam Lazaro Jacob Twange kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).
Rais Samia Suluhu Hassan
Uteuzi wa Twange umetangazwa Mei 7,2025 kupitia taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi, Dk. Moses Kusiluka, iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Sharifa Nyanga.

Twange aliyewahi kuwa Naibu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA),anachukua nafasi ya Mhandisi Nyamo-Hanga ambaye alifariki dunia kwa ajali ya gari.

Taarifa zaidi soma kiambatanisho chini;


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Kapteni Traole afuata huduma za afya nchini

Wawekezaji wa Oman watua nchini, wateta na NHC kuchochea mapinduzi sekta ya makazi

Moshi mweusi watokea Vatican, moshi mweupe wasubiriwa kwa hamu