Makardinali 133 wajifungia kusaka Papa mpya
-Ni Papa wa 267 wa Kanisa Katoliki
Mwandishi Wetu, daimatznews@gmail.com
Takriban Makardinali 133 wa Kanisa Katoliki duniani, leo Mei 7, 2025 wanaanza mchakato wa kumtafuta Papa mpya.
Papa huyo mpya ndiye atakayerithi nafasi hiyo ya kuliongoza Kanisa Katoliki, kufuatia kifo cha Papa Francis Aprili 21,2025 mjini Vatican.
Mkutano huo maarufu kwa jina la Conclave unafanyika katika Kanisa dogo la Sistine Chapel, Vatican City, makao makuu ya kanisa hilo, ambapo makardinali hao kutoka nchi mbalimbali hujifungia wakisali na kuendesha mchakato huo ili kumpata kiongozi wao.
Kardinali Protas Rugambwa, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Tabora, pia anashiriki mkutano huo wa kihistoria ndani ya Kanisa Katoliki kumchagua Papa.
Papa hutambulika pia kama Halifa wa Mtume Petro, anayeaminika na Kanisa Katoliki kuwa ndiye kiongozi wa kwanza wa kanisa hilo, aliyechaguliwa na Yesu Kristo, kuchunga kundi la wanafunzi wake.
Maoni
Chapisha Maoni