Mkenda amebainisha hayo jijini humo wakati akizungumza na waandishi wa habari na kuitaka VETA kutengeneza mpango kazi katika kushirikiana na wadau mbalimbali ili kuwezesha vijana wenye mafunzo ya ufundi stadi kuwa uwanja mpana kujiajiri na kuleta maendeleo nchini
Amesema kuwa kuna mafundi ambao hawana hawajapita katika vyuo vya VETA lakini ni wabunifu ambao nao washirikishwe kupata mafunzo na kutoa ujuzi huo kwa wanafunzi waliopo na baadae kuungana katika uzalishaji na bidhaa pamoja na ufundi kwenye sekta mbalimbali.
Waziri Mkenda amesema shughuli mbalimbali zitafanyika katika kuelekea kwenye kilele cha maadhimisho hayo, ikiwemo kutoa huduma kwa jamii, kuendesha maonesho ya teknolojia na ujuzi, pamoja na kutoa tuzo na vyeti vya heshima kwa watu mbambali kwa mchango wao katika shughuli za maendeleo ya Ufundi Stadi nchini.
Amesema mwaka huu wataadhimisha miaka 30 ya VETA ambayo ilianzishwa kwa Sheria ya Bunge mwaka 1994 na kuanza kazi rasmi mwaka 1995. Kabla ya VETA kulikuwa na Idara ya Mafunzo na Majaribio ya Ufundi Stadi (NVTD) katika Wizara ya Kazi na Ustawi wa Jamii ambayo ilianzishwa mwaka 1975.
Kwamba Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni Ukuzaji Stadi na Ubunifu kwa Maendeleo ya Jamii na Taifa’.
Amebainisha kuwa kwa kipindi cha miongo mitatu ya VETA imeendelea kuwa mstari wa mbele katika kuwajengea Watanzania uwezo wa kujiajiri, kuajiriwa, na kuchangia katika kukuza uchumi wa nchi.
Aidha amesema kuwa VETA imekuwa na mafanikio na kuwa taasisi muhimu inayochangia rasilimali watu yenye ujuzi inayohudumu katika sekta mbalimbali, ikiwemo Viwanda, Kilimo, Ujenzi, Teknolojia, Nishati na huduma na Utalii.
Amesema kuwa, maadhimisho hayo pia ni fursa ya kipekee kwa jamii kusherehekea mchango wa ufundi stadi katika maendeleo ya nchi kiuchumi na kijamii, huku tukijipanga kuimarisha sekta ya ufundi stadi ili kuendana na mabadiliko ya kiteknolojia na mahitaji ya soko la ajira.
“Maadhimisho haya ya miaka 50 ya utoaji elimu na mafunzo ya ufundi stadi pamoja na miaka 30 ya VETA yanakuja wakati Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameagiza kukamilishwa ujenzi wa vyuo vya VETA vya hadhi ya kimkoa, katika mikoa yote ambayo haina vyuo vya VETA na vyuo vya VETA vyenye hadhi ya kiwilaya katika wilaya zote ambazo hazina vyuo hivyo.
Pia mesema kwa sasa VETA inakamilisha ujenzi wa chuo chenye hadhi ya Mkoa cha VETA kwa Mkoa wa Songwe na tunaendelea na ujenzi wa vyuo 64 katika wilaya 64 ambazo zilikuwa hazina vyuo hivyo.
“Nitumie fursa hii kuwakaribisha wadau wote katika maadhimisho haya yanayoendelea nchini na upekee katika kilele cha yatayofanyika jijini Dar es Salaam ili tujionee na kujadili umuhimu wa elimu na ujuzi kulingana na mabadiliko ya Sera ya Elimu na Mafunzo yam waka 2014 toleo la 2023,” amesema Profesa Mkenda
0 Maoni