Mkurugenzi Tanesco ahimiza matumizi

 Hussein Ndubikile, daimatznews@gmail.com

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga amewahimiza Watanzania kutumia fursa ya uwepo wa umeme katika kila Kijiji na kutumia nishati hiyo kupikia, ili kupunguza gharama pamoja na kutunza mazingira akieleza kwamba umeme ni nishati nafuu zaidi kupikia
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga, akisisitiza jambo alipozungumza katika kongamano la Wananwake kuhamasisha matumizi ya Nishati Sani na umeme.

 Gissima ameyasema hayo jijini humo katika Kongamano la Wanawake la Kuhamasisha Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia ya Umeme lililofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City   ambapo Mgeni rasmi alikuwa ni Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dk. Doto Biteko ambae aliambatana na Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga.

“Kwa sasa umeme umefika kwenye kila kijiji hivyo ni vizuri kwa Watanzania kufahamu ya kuwa wana fursa ya kupika kwa kutumia nishati safi ya umeme. Tunaendelea kuwahimiza na kuwafahamisha ya kuwa umeme ni nishati safi zaidi na nafuu zaidi ya kupikia”, amesisitiza Gissima.

Amesema  kuwa matumizi ya umeme kupikia yanawapunguza gharama watumiaji na madhara wanayoweza kupata wakitumia nishati nyingine.

Kwa upande wake, Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko amelihimiza shirika hilo kuendelea kutoa elimu ya nishati safi ya kupikia kwa jamii hususan wanawake.

Dk. Biteko amelipongeza shirika hilo kwa kuwapa nafasi wanawake kwenye ajira na kuongeza kuwa idadi ya waajiriwa wanawake imeongezeka.

Pia amelitaka shirika hilo kuhakikisha linaendelea kuwaunganishia huduma ya umeme wananchi pamoja na kupatikana kwa uhakika wa huduma ya umeme.

Katika hatua nyingine, Waziri Dk. Biteko ameitaka TANESCO kutoa majiko ya umeme kwa waajiriwa wanawake ili kuendelea kuhamasisha matumizi ya umeme kupikia

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Kapteni Traole afuata huduma za afya nchini

Wawekezaji wa Oman watua nchini, wateta na NHC kuchochea mapinduzi sekta ya makazi

Moshi mweusi watokea Vatican, moshi mweupe wasubiriwa kwa hamu