Mvutano waibuka kesi ya heroin

-Washtakiwa wapinga kielelezo

-Jamhuri wakwama kutoa hadharani 

Mwandishi Wetu, daimatznews@gmail.com 

Mvutano umeibuka mahakamani wakati upande wa mashtaka katika kesi ya kusafirisha heroine kilo 1.02  inayomkabili Maliki Maliki na wenzake watatu 'ukikabwa koo', na mawakili wa utetezi waliopinga kielelezo kupokelewa, wakidai ni batili.

Mvutano huo wa kisheria uliibuka Februari 28,2025 katika Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi mbele ya Jaji Godfrey Isaya wakati shahidi alipoomba kutoa kielelezo.

Shahidi Inspekta Msaidizi wa Polisi, John Marwa akiongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mafuru Moses alidai Machi 24 mwaka 2022 alienda kufanya upekuzi baada ya kupewa mamlaka ya kufanya hivyo.

Kibali cha kufanya upekuzi kilijazwa Machi 24 mwaka 2022 saa tisa usiku aliomba kutoa Mahakamani kama ushahidi.

Wakili wa utetezi Nehemiah Nkoko alipinga alidai hana sifa ya kufanya hivyo na si miongoni mwa vielelezo ambavyo Sheria ya Uhujumu Uchumi na Sheria ya Kudhibiti dawa za kulevya inakitambua.

Alisema afisa anayefanya upekuzi kama anatoka taasisi nyingine lazima apate mamlaka kwa Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kuzuia Dawa za Kulevya.

"Afisa kutoka Taasisi nyingine anatakiwa haraka aripoti kwa afisa kutoka Mamlaka ya Kudhibiti dawa za kulevya lakini fomu anayotaka kutoa shahidi ni kutoka Jeshi la Polisi .

"Rai yetu kwa sababu shahidi si afisa wa Mamlaka na hajapewa mamlaka ya kufanya hivyo hana sifa ya kutoa kielelezo hiki,"alisema Nehemiah.

Alisema shahidi anasema alipewa kibali saa tisa usiku lakini hati yenyewe inaeleza saa tatu asubuhi.

Aliomba Mahakama isipokee kielelezo hicho kwa sababu ni batili.

Akijibu Wakili Mafuru aliomba Mahakama ipokee kielelezo na itupilie mbali pingamizi za upande wa utetezi kwa madai hazina mashiko.

Shauri liliahirishwa hadi wiki ijayo kwa ajili ya uamuzi na kuendelea na usikilizwaji ushahidi

Washtakiwa ni Maliki, Iddi Nassoro, Ally Maliki na Mwinyi Mgazija.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Kapteni Traole afuata huduma za afya nchini

Wawekezaji wa Oman watua nchini, wateta na NHC kuchochea mapinduzi sekta ya makazi

Moshi mweusi watokea Vatican, moshi mweupe wasubiriwa kwa hamu