Serikali yawekeza Sh. trilion 1.29 huduma za afya

 Hussein Ndubikile, daimatznews@gmail.com

Serikali imewekeza Sh trillioni moja na bilioni 298 ili kuboresha huduma za afya nchini,na kuhakikisha Watanzania wanapata dawa na vifaa tiba vya kutosha.

Msemaji Mkuu wa Serikali, Greyson Msigwa akizungumza na waanishi wa habari jijini Dar es SalaamleoMachi 3, 2025.

Msemaji Mkuu wa Serikali Greyson Msigwa amebainisha hayo leo  Machi 3,2025, wakati akizungumza na wanahabari jijini Dar es salaam akieleza kuwa hatua hiyo inalenga kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya.

Msigwa ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ameeleza kuwa mageuzi makubwa yaliyofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan katika sekta ya afya yameleta matokeo makubwa, ikiwemo kupungua kwa vifo vya akinamama wanaojifungua kutoka 556 hadi 104 ndani ya miaka minne ya uongozi wake.

" Lengo la Serikali ni kupunguza vifo hivyo hadi asilimia 70 ifikapo mwaka 2030. Lengo hili litafanikiwa kwa kiwango kikubwa kwani Rais Dk.Samia amewekeza jitihada za makusudi katika kuboresha huduma za afya kila kona ya nchi hii," amesema Msigwa.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Sanamu ya Bikira Maria yaonekana ndani ya Hifadhi ya Taifa Saadani

Kapteni Traole afuata huduma za afya nchini

Wawekezaji wa Oman watua nchini, wateta na NHC kuchochea mapinduzi sekta ya makazi