Rais Samia kuzindua Bawe Hotel
Mwandishi Wetu,daimatznews@gmail.com
Zanzibar,
Rais Samia Suluhu Hassan, muda mfupi ujao leo Januari 7,2025 atazindua Hoteli Bawe ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 61 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar.
![]() |
Baadhi ya wananchi wa Zanzibar wakifuatilia uzinduzi wa Bawe Hotel, Januari 7, 2025. |
Mapinduzi ya Zanzibar yalifanyika Januari 12, 1964, ambapo yaliuondoa madarakani utawala wa kisultani na wazanzibari kushika hatamu ya kuliongoza taifa lao, chini ya Hayati Mzee Abeid Aman Karume. Sherehe za Mapinduzi mwaka huu 2025, zinabebwa na kauli mbiu; Amani, Umoja na Mshikamano huleta Maendeleo.'
Tayari Rais Samia amewasili eneo hilo kwa ajili ya kazi hiyo, ambapo alitanguliwa na mwenyeji wake, Dk. Mwinyi
Uzinduzi huo utafanyika kisiwni Bawe, moja ya maeneo maalum ya visiwa vidogo yaliyotengwa kwa ajili ya uwekezaji na Mamlaka ya Uwekezaji visiwani Zanzibar, (ZIPA).
Rais Samia atazindua hoteli hiyo akiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, ambaye uwekezaji katika visiwa vidogo zaidi ya 17 ni sehemu ya mkakati wake wa kuwainua wazanzibari kiuchumi.
Uwekezaji katika Kisiwa cha Bawe umefanywa na mwekezaji kutoka Italia, Kampuni ya Bawe Retreat Limited.
Hoteli hiyo ina majengo 129 yanayojumuisha vyumba vya kulala wageni, villa, vyumba vya kifahari na fukwe za bahari.
Maoni
Chapisha Maoni