Mama Ongea na Mwanao ywasaidia watu wenye ulemavu, Meya Kumbilamoto ataka waungwe mkono
Na Hussein Ndubikile,daimatznews@gmail.com
Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao, imeukaribisha Mwaka Mpya wa 2025 kwa kutoa misaada mbalimbali wenye ulemavu na mahitaji maalum.Meya wa Jiji hilo, Omari Kumbilamoto akizungumza wakati wa hafla hiyo ukumbi wa Karimjee Dar es Salaam
Akizungumza jijini Dar es Salaam katika hafla ya utoaji msaada huo jijini Dar es Salaam, Meya wa Jiji hilo, Omari Kumbilamoto ametoa rai kwa wadau mbalimbali kuunga mkono juhudi za taasisi hiyo katika kuyashika mkono makundi ya watu wenye mahitaji maalum.
"Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao ambayo Steve Mangele ni Mwenyekiti, inafaa kuigwa Kwa hayo inayoyafanya kwa kuwasapoti watu wenye ulemavu kwa kutoa zawadi mbalimbali," amesema Kumbilamoto.
Amesema Serikali imejipambanua kuhakikisha inatoa shilingi billion 5 kwa kundi la wenye ulemavu.
Mwenyekiti wa Taasisi hiyo, Steven Mengele 'Steve Nyerere', amesema kundi hilo ni muhimu sana na mwaka huu ni mwaka wa tatu toka kuazishwa Kwa utaratibu wa kulishika mkono kundi hilo.
![]() |
Baadhi ya watu wenye ulemavu wakikabihiwa viti mwendo wakati wa hafla hiyo. |
"Rais wetu Mama Dk. Samia ameamua kutushika mkono, hivyo tumekuwa tukitembea maeneo mbalimbali ya Tanzania kwa kila mkoa kuhakikisha tunakutana na watu wenye uhitaji kwa kuwapa zawadi mbalimbali ikiwemo viti mwendo 50, pamoja na kukarabati madarasa yao," amesema Nyerere.
Amesema kuwa lengo la kulishika mkono kundi hili ni ili liweze kufurahia maisha kama watu wengine, ndiyo maana wanakutana nao na kula na kucheza nao.
Maoni
Chapisha Maoni