Na Hussein Ndubikile,daimatznews@gmail.com
Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa masuala ya uchukuzi inandaa mapendekezo ya kutunga Sheria ya Bodi ya Uchukuzi kwa lengo la kuwatambua na kuwasajili wana taaluma hao.
Kauli hiyo imetolewa jijini humo na Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile pichani juu, katika Mahafali ya 40 ya Chuo Cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), mkoani Dar es Salaam, Desemba 22,2024.

"Bodi hiyo itakuwa na jukumu la kusimamia weledi na maadili ya watalaam wa uchukuzi Tanzania Bara," amesema Kihenzile na kuongeza;
"Uanzishwaji wa bodi hiyo una lengo la kuhakikisha kazi zote za usafirishaji zinasimamiwa na watu wenye taaluma stahiki."
Akizungumzia kuhusu NIT, Naibu Waziri. Kihenzile amesema Serikali itaendelea kukiwezesha Chuo cha Taifa cha Usafirishaji kwa kukiboreshea miundombinu yake ya kufundishia ili kuhakikisha kinatimiza majukumu yake ya kuandaa wataalam, kufanya tafiti na kutoa ushauri wa kitaalamu katika sekta ya uchukuzi kwa maendeleo endelevu ya taifa.

Kihenzile ametoa rai kwa wadau mbalimbali wa usafiri na usafirishaji kuunga mkono jitihada za Chuo katika kuwapatia nafasi za mafunzo kwa vitendo wanafunzi na kuendeleza bunifu zinazozalishwa chuoni ili zitumike kwa maendeleo ya nchi.
Ametoa rai kwa wadau na wafaidika wa shughuli za chuo, taasisi za umma na binafsi kuunga mkono jitihada za chuo hicho katika kupata nafasi za mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi kuendeleza bunifu zinazozalishwa chuoni hapo ili ziweze kutumika kwa maendeleo ya nchi.

“Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo NIT ipo katika hatua za kuandaa mapendekezo ya kutunga sheria ya Bodi ya usajili wa wataalam wa uchukuzi lengo likiwa ni kuwa tambua, kuwasajili na kusimamka weledi wa maadili ya wataalam wa uchukuzi Tanzania Bara ili kuhakikisha kazi zote za usafirishaji zinasimamiwa na watu wenye taaluma stahiki” amesema Naibu Waziri huyo.
Awali, Mkuu wa Chuo cha NIT, Mhandisi Dk. Prosper Mgaya amesema katika mahafali hayo wahitimu 4,176 wametunukiwa vyeti katika ngazi mbalimbali kati yao wanaume ni 2,581 na wanawake 1,595.

Akizungumzia changamoto amesema, chuo hicho kimekuwa na mikakati ya kukabiliana nazo zikiwemo za miundombinu, upungufu wa rasilimali watu na ongezeko la udahili wa wanafunzi kwa kuweka mikakati mbalimbali.
Amesema pamoja na mabweni chuo kinajenga ofisi,madarasa na karakana ambapo jumla ya majengo matatu yanajengwa na yanatarajiwa kukamilika Februari 2025 ambapo ujenzi huo unafadhiliwa na Benki ya Dunia kupitia mradi wa EASTRIP.

Amesema chuo pia kinaanzisha kampasi mpya mkoani Lindi na Kilimanjaro ili kupunguza msongamano wa wanafunzi katika kampasi ya Dar es Salaam na kuhusu rasilimali watu ili kukabiliana nalo wanaendelea kuomba vibali vya ajira Serikalini ili kupunguza matumizi ya wahadhili wa muda.
0 Maoni