Serikali yaagiza shule nchini zijengewe uzio kulinda wanafunzi
Mwandishi Wetu, daimatznews@gmail.com
Serikali imeziagiza halmashauri zote nchini kujenga uzio katika shule ili kuboresha na kulinda usalama kwa wanafunzi na rasilimali za shule hizo.
![]() |
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Walimu Wakuu wa Shule za Sekondari na Msingi jijini Dodoma,Desemba 12, 2024 |
Agizo hilo limetolewa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Desemba 12,2024 jijini Dodoma ambapo ameelekeza wafanye hivyo kwa kutumia sehemu ya mapato yao ya ndani.
Ametoa agizo hilo wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Chama Cha Walimu Wakuu wa Shule za Sekondari na za Msingi Tanzania, katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete, jijini humo
![]() |
Walimu wakuu wa shule za msingi na sekondari wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika ufunguzi wa mkutano wao mkuu wa mwaka jijini Dodoma Desemba 12, 2024. |
Akizungumza katika mkutano huo, Rais wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Walimu Wakuu wa Shule za Sekondari na za Msingi Tanzania, Denis Otieno amemshukuru Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuingiza fedha nyingi katika ujenzi wa miundombinu ya shule nchini na kutatua changamoto mbalimbali kwenye sekta ya elimu nchini.
Mkutano huo umekutanisha walimu wakuu wa shule za sekondari na msingi ambapo wamejadili masuala mbalimbali yanayohusu wao binafsi nauboreshaji elimu nchini.
![]() |
Baadhi ya walimu wakuu wakifuatilia mkutano wao unaofanyika Dodoma Desemba 2024 |
Maoni
Chapisha Maoni