Serikali kuanzisha sheria usimamizi wa huduma Ustawi wa Jamii

Na Hussein Ndubikile, daimatznews@gmail.com

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake, Watoto na Makundi Maalumu, Dk. Dorothy Gwajima, amesema wizara yake kwa kushirikiana na wizara nyingine, inajiandaa kuanzisha sheria itakayohusu usimamizi wa huduma za kada ya ustawi wa jamii.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake, Watoto na Makundi Maalumu, Dk. Dorothy Gwajima, akizungumza katika Mahafali ya 48 ya Chuo cha Ustawi wa Jamii, Kijitonyama na Mahafali ya Saba, Tawi la Kisangara jijini Dar es Salaam, Desemba 12,2024.

Akizungumza katika Mahafali ya 48 ya Chuo cha Ustawi wa Jamii, Kijitonyama na Mahafali ya Saba, Tawi la Kisangara yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, Dk. Gwajima amesema:

"Sheria hiyo itainua huduma za ustawi wa jamii, kulinda taaluma na kutoa fursa kwa watoa huduma binafsi kusajiliwa na kupata vibali vya kufanya kazi."

Amesisitiza kuwa huduma hizi zinakutana na changamoto, ikiwemo mauaji, na kwamba maofisa wa ustawi wa jamii watakuwa mstari wa mbele kupambana na hali hiyo. 

Gwajima ametoa mfano wa tukio la uhalifu lililotokea Dodoma, ambapo maofisa wa ustawi walifanya kazi usiku kuchunguza na kutatua tatizo la mtoto aliyeumizwa.

Wahitimu wa Mahafali ya 48 ya Chuo cha Ustawi wa Jamii, Kijitonyama na Mahafali ya Saba, Tawi la Kisangara wakifuatilia hafla hiyo jijini Dar es Salaam, Desemba 12,2024.

.
“Juzi saa 5:47 usiku nilipokea ujumbe wa maneno kutoka Dodoma, Mtaa wa Iyumbu kwamba kuna mtoto anapigwa, Mungu alinisaidia nilikuwa macho ningepeleka wapi hili sawala? Mtu wa kwanza niliyemwamsha alikuwa Ofisa Ustawi wa Jamii wa Dodoma,” amesema na kuendelea:

“Naye akamtafuta mtu wa Dawati la jinsia wakafanya kazi usiku, hadi katika eneo la tukio walikuta mtoto ameumizwa yeye na binti wa kazi, kufuatilia ni mtoto wa ndugu yake alimchukua kwa jili ya kusoma.”

Hata hivyo, amesema baada ya uchunguzi wamegundua wahusika wana tatizo la kisaikolojia ambalo lilikuwa linahitaji huduma kutoka kwa wahusika wa masuala hayo.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Sanamu ya Bikira Maria yaonekana ndani ya Hifadhi ya Taifa Saadani

Kapteni Traole afuata huduma za afya nchini

Wawekezaji wa Oman watua nchini, wateta na NHC kuchochea mapinduzi sekta ya makazi