Hot Posts

6/recent/ticker-posts

Kigoma, minara ya mtandao 47, watu laki nane wanufaika

Mwandishi Wetu, WHMTH, Kigoma

Takriban  Watanzania 866,352, wamenufaika na huduma bora za mawasiliano katika Mkoa wa Kigoma, kutokana na mradi wa minara ya simu 47 iliyojengwa na kuanza kutumika mkoani humo.

Baadhi ya wananchi wa Mkoa wa Kigoma, wakifuatilia mkutano wa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye na watendaji wa Mkufo wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Julai 15, 2024.

Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Justina Mashiba, amebainisha hayo Julai 15, 2024, wakati akitoa taarifa ya utendaji wa mfuko huo katika Mkoa wa Kigoma, mbele ya Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye.

Mashiba amesema, minara hiyo imejengwa kwa teknolojia ya 2G, 3G na 4G, kwa ruzuku iliyotolewa na UCSAF, kwa makubaliano na watoa huduma, imegharimu jumla ya Shilingi Bilioni 6.3.

Ametaja wilaya zilizofaidika na minara hiyo pia minara iliyojengwa, kwenye mabano, kuwa ni Buhigwe (6), Kakonko (12), Kasulu DC (6), Mji wa Kasulu (5), Kibondo (8), Kigoma DC (2) na Uvinza (8). 

Mashiba amesema kuwa Mkoa wa Kigoma ni kati ya mikoa 26 Tanzania Bara, itakayonufaika na mradi wa minara 758 inayoendelea kujengwa nchi nzima na inayotarajiwa kuwafikia Watanzania zaidi ya milioni 8.5 itakapokamilika mwanzoni mwa mwaka 2025. 

 Amezitaja wilaya za Mkoa wa Kigoma inakojengwa minara hiyo na idadi ya minara kuwa ni Kasulu (3), Kibondo (3) na Uvinza (2), na kutaja ruzuku ya Serikali kupitia UCSAF iliyotumika kwa minara hiyo kuwa ni Shilingi Bilioni 1.38. 

Kwa mujibu Mashiba kufikia mwishoni mwa Juni 2024, jumla ya minara mitatu ya mradi hiyo ilishakamilika na kuwashwa, ikivinufaisha vijiji kadhaa, vikiwemo Kijiji cha Katete wilayani Uvinza, na Bunyango na Kumbanga wilayani Kibondo. 

UCSAF ni taasisi ya Serikali iliyoanzishwa kwa lengo la kufikisha huduma za mawasiliano vijijini na mijini, kusiko na mvuto wa kibiashara, kwa kushirikiana watoa huduma za mawasiliano, zikiwemo kampuni za Airtel, Halotel, Tigo, TTCL na Vodacom.

Tangu uipoanziswa mwaka 2009 hadi mwaka 2024 UCSAF imeshazifikia kata 1,349 ambako minara 1,481 ya mawasiliano imejengwa na kunufaisha wananchi takriban milioni 16.59 nchi nzima.

Chapisha Maoni

0 Maoni