Kunani tarehe 29 kwa Rais Dk. Samia CCM?

- Aliamua ya Chongolo, ameamua ya Kinana Mwandishi Wetu, daimatznews@gmail.com Sijui unakumbuka.. au najua? Kama hukumbuki au hujui, nitakuwekea sawa kumbukumbu kuhusu maamuzi makubwa, mazito mawili ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa (CCM), Rais Dk, Samia Suluhu Hassan ndani ya chama hicho tawala. Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Dk. Samia Suluhu Hassan Ni hivi, kumbukumbu zinaonyesha kuwa tarehe 29 ndiyo CCM ilitangaza maamuzi magumu ya Mwenyekiti wake huyo wa Taifa, yaliyobeba mustakabali wa chama hicho tawala ndani ya miezi minane, Novemba 29,2023 hadi Julai 29,2024. Tarehe hiyo, ndipo alitangaza kuridhia kujiuzulu kwa Daniel Chongolo aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, mwaka uliopita 2023 na mwaka huu 2024, ameridhia kujiuzulu kwa Makamu Mwenyekiti wa CCM, Kanali Mstaafu, Abdulrahman Kinana. Taarifa ya CCM ya jana Julai 29, 2024 imeeleza kwamba Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, ameridhia ombi la Makamu Mwenyekiti wake, Kinana kujiuzulu wa...