Hot Posts

6/recent/ticker-posts

Shinyanga yasajili laini milioni mbili za simu, kitaifa zafikia bilioni 72

Mwandishi Wetu,WHMTH, Shinyanga 

Wakati laini za simu zilizosajiliwa nchi nzima zikifikia milioni 72.4, Mkoa wa Shinyanga pekee, zimesajiliwa laini 1,966,528 ambazo ni sawa na asilimia 2.71 ya laini zote nchini.

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe Nape Nnauye (kulia) akiwa pamoja na Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Justina Mashiba  kwenye Boti ya Mwendokasi  Ziwa Viktoria, kuelekea kukagua mnara wa VODACOM uliopo katika Kata ya Chifunfu, Kijiji cha Chifunfu, Kisiwa cha Lyakanyasi, Sengerema mkoani Mwanza Julai 18,2024 katika ziara yake ya ukaguzi wa ujenzi wa minara ya Mawasiliano mkoani humo.

Mkurugenzi wa Leseni na Ufuatiliaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Wakili John Daffa amebainisha hayo leo Julai 19, 2024 wakati akitoa wasilisho la hali ya huduma ya mawasiliano kwa mkoa huo, mbele ya Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Moses Nnauye (Mb), na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Anamringi Macha.

“Ukuaji wa usajili wa laini za simu umeongezeka kwa asilimia 19.8 kutoka Juni 2022 hadi Machi 2024 ambapo jumla ya laini za simu zilizosajiliwa ni 1,966,528 kutoka line 1,641,547,” amesema Wakili Daffa, katika mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa.

Amesema, kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022, Shinyanga ina wakazi 2,241,299 na kwa ulinganifu wa idadi ya watu na laini za simu ni sawa na asilimia 87.74.

Kuhusu hali ya ufikiwaji wa huduma za mawasiliano katika Mkoa, Wakili Daffa amesema, umeimarika kwani wanaopata mawasiliano ya 2G ni asilimia 99.5, 3G ni asilimia 99, 4G asilimia 96.66 na 5G ni 2.68.

Mkurugenzi wa Leseni na Ufuatiliaji kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Wakili John Daffa wakati akitoa wasilisho la hali ya huduma ya mawasiliano kwa mkoa huo, mbele ya Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe Nape Moses Nnauye (Mb), na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Anamringi Macha

Kuhusu hali ya upatikanaji wa mawasiliano ya simu na inteneti mkoani Shinyanga, Wakili Daffa amesema, ili huduma ziweze kupatikana ni lazima miundombinu ijengwe na tayari minara 257 imejengwa hadi kufikia mwaka 2024. 

Wakili Daffa amesema, TCRA inaimarisha ushirikiano na wadau katika kutatua changamoto hususani usalama wa mitandao inayochangiwa na uelewa mdogo wa watumiaji wa huduma hizo, uhalifu mtandaoni na mawasiliano hafifu kwa baadhi ya vijiji.

Amesema, kwa kutambua kuwa Sekta ya Mawasiliano ni sekta wezeshi inayokuwa kwa kasi na kufungua fursa mbalimbali, usimamizi thabiti unafanyika ili kuongeza mchango wake katika uchumi na maendeleo ya Taifa.

Chapisha Maoni

0 Maoni