Hot Posts

6/recent/ticker-posts

Kimbunga cha Rais Samia chang'oa vigogo wengine sita

 Mwandishi Wetu, daimatznews@gmail.com

Siku chache baada ya kuwaondoa madarakani mawaziri watatu wa Serikali yake, akiwamo aliyekuwa Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia na Habari, Nape Nnauye, kimbunga cha Rais Dk Samia Suluhu Hassan safari hii kimewakumba watendaji sita wa taasisi zilizokuwa chini ya wizara hiyo iliyoongozwa na Nape.

Rais Dk, Samia Suluhu Hassan akisistiza jambo katika moja ya mikutano yake.

Taarifa iliyotolewa leo Julai 23, 2024 na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais,Ikulu, Sharifa Nyanga ikinukuu taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dk. Moses Kusiluka imeeleza kuwa Rais Samia ametengua uteuzi wa viongozi mbalimbali.

"Waliotenguliwa ni kama ifuatavyo;..Zuhura Sinare Muro, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurgenzi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) na Mhandisi Peter Rudolf Ulanga, Mkurugenzi wa TTCL," imeeleza taarifa hiyo ikimnukuu Balozi Dk. Kusiluka na kutaja wengine waliotenguliwa nyadhifa zao kuwa ni:

"Brigeia Mstaafu Yohaya Ocholla Mabongo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurgenzi ya Shirika la Posta Tanzania na Maharage Aly Chande, Postamasta Mkuu, Shirika la Posta Tanzania."

Wengine waliotenguliwa nyadhifa zao na Rais Samia leo ni pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurgenzi ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko huo, Justina Mashiba.


Chapisha Maoni

0 Maoni