Mwandishi Wetu,daimatznews@gmail.com Tanzania imepiga hatua isiyosahaulika katika historia ya maendeleo yake, baada ya kikosi cha wawekezaji wa ngazi ya juu kutoka Ufalme wa Oman, kufanya ziara nchini na kukutana na uongozi wa Shirika la Nyumba Tanzania (NHC), wakifungua fursa kubwa za mabadiliko makubwa katika sekta ya nyumba na maendeleo ya miji nchini. Ujumbe wa Wawekezaji kutoka Oman(kulia) ukiwa katika mkutano na uongozi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), (kushoto), makao makuu ya shirika hilo jijini Dar es Salaam Mei 20,2024. Ujumbe huo uliongozwa na Balozi wa Oman nchini Tanzania, Saud Al Shidha, ulikuwa na malengo kadhaa ya kukuza ushirikiano wa kiuchumi ikiwamo kuanzisha mabadiliko ya kimkakati, yatakayochochea ukuaji wa sekta ya makazi kwa njia ya ubia wa kimataifa. Katika kikao cha kihistoria kilichofanyika Makao Makuu ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) – Kambarage House, ujumbe wa Oman ulipokelewa na Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Hamad Abdallah, pamoja na viongozi waandamizi w...
Maoni
Chapisha Maoni