Hot Posts

6/recent/ticker-posts

Ni haki ya kila mwananchi kufaidi huduma ya mtandao-Nape

 -Minara 760 ya mawasiliano kukamilika 2025, Wananchi 8500 kunufaika

Mwandishi Wetu,  daimatznews@gmail.com

Jumla ya minara 758 ya mawasiliano inajengwa nchini ikitarajiwa kukamilika mwaka 2025 na kuwanufaisha wananchi 8,512, 952 wa vijijini kwa kupata huduma ya mawasilino hasa mitandao, huku Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Mnauye akisema ni haki ya kila mwananchi kunufaika na huduma hizo.

 Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Mnauye akisisitiza jambo, wakati wa mkutano wake na uongozi wa Mkoa wa Kigoma leo Julai 15, 2024.

Kutekelezwa kwa mradi huo mkubwa kunafanyika katika mikoa 26 ya Tanzania Bara inayojumuisha wilaya 127, vijiji 1,407 vilivyo katika kata 713, kumebainishwa leo Julai 15, 2024 mkoani Kigoma, wakati Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye akipokea taarifa za mawasiliano alipofanya ziara ya siku moja ya kikazi mkoani humo.

Katika ziara yake mkoani humo, Nape amekagua ujenzi wa minara hiyo na kusema:
x

“Kukamilika kwa minara hiyo kutatoa fursa kubwa kwa wananchi wa vijijini ya kupata mawasiliano kama wananchi wa maeneo mengine katika ulimwengu wa uchumi wa kidigitali. Hiyo ni haki yao kama ilivyo kwa wananchi wengine.”

 Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Mnauye (wa sita kulia), akiwa katika picha ya pamoja na uongozi na watendaji mbalimbali wa mkoa wa Kigoma alipofanya ziara ya kikazi leo Julai 15, 2024.

Nape amefanya ziara kama hiyo katika mikoa ya Shinyanga, Geita na Kagera.

Chapisha Maoni

0 Maoni