Mwandishi Wetu,daimatznews@gmail.com
Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), limeipongeza Klabu Waandishi wa Habari Dar es Salaam (DCPC) kwa ushirikiano wa kikazi na kimkakati, iliouonyesha kwa shirika hilo kipindi chote cha mwaka 2023.
Pongezi hizo zimetolewa leo Desemba 29, 2023 na Mkurugenzi wa TTCL, Mhandisi Peter Ulanga kupitia kwa maofisa uhusiano wa shirika hilo, Adeline Berchimance na Rehema Nyangasa waliotembelea ofisi za DCPC Mtaa wa Samora, ambapo wamewasilisha zawadi na ujumbe maalum kutoka kwa Mhandisi Ulanga, aliyesema klabu hiyo imefanya vizuri katika kuandika habari za shirika hilo na kulitangaza.
Naye Kaimu Meneja Uhusiano wa TTCL, Edwin Mashaz ameishukuru DCPC na kuiomba idumishe ushirikiano, akitoa rai kwa waandishi wa habari hasa wa klabu hiyo, wasisite kuwasiliana naye ili kupata ufumbuzi kuhusu changamoto yoyote inayohusu kampuni hiyo.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa DCPC, Fatma Jalala ameishukuru TTCL na kuahidi kudumisha uhusiano, hasa katika kuitangaza TTCL kupitia mitandao ya kijamii inayomiliki ili kuwaonyesha watumiaji kuwa kampuni hiyo ndio Baba wa mawasiliano na wengie wanafuata.
"Wote tuna lengo moja kuunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan za kujenga nchi na maendeleo ya wananchi," amesema Fatma
0 Maoni