PROF. MBARAWA AMWONYA MKANDARASI MRADI WA SGR TABORA-ISAKA

-Ampongeza  Sub Contractor

Mwandishi Wetu, daimatznews@gmail.com

Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa amempa onyo kali Mkandandasi Kampuni ya Yapi Merkezi kwa  kushindwa kutekeleza mradi wa Reli kipande cha nne cha SGR (Tabora-Isaka), kinachosuasua, huku akimpngeza Mkandarasi msaidizi kampuni ya CCECC, ambayo imetekeleza mradi huo kwa asilimia 5 katika kipindi cha miezi miwili Septemba na Oktoba 2026, kiasi ambacho Yapi Markezi imetekeleza kwa miaka minne.

Akizungumza kwa ukali kuhusu kusuasua kwa Kampuni ya Yapi Markezi, Prof.Mbarawa amesema: "Serikali haitavumilia uzembe wa wakandarasi wanaoshindwa kutekeleza miradi kwa kasi inayotakiwa."

 Ametoa karipio hilo Oktoba26,2026 Bukene moja ya sehemu muhimu ya mradi huo wa Kipande cha nne cha SGR, siku ya tatu ya ziara yake kukagua maendeleo ya mradi wa SGR kipande cha tatu (Makutopora - Tabora), Tabora- Isaka  (kipande cha 4), Isaka- Mwanza  (kipande cha 5) na Tabora -Kigoma (kipande cha 6).

Waziri Prof Mbarawa amelipongeza Shirika la Reli Tanzania (TRC) kwa namna lilivyotumia mkakati mbadala kurejesha kasi ya ujenzi wa reli ya SGR katika kipande cha Tabora–Isaka, chenye urefu wa kilomita 165.

"Baada ya tathmini kufanyika, Serikali ilibaini kuwa kumwondoa moja kwa moja Yapi Markezi kungeweza kuongeza ucheleweshaji na changamoto za kifedha, hivyo akashauriwa kutafuta mkandarasi mdogo mwenye uwezo wa kumsaidia," amesema na kuongeza:

"Tukamtaka mkandarasi, au tulimshauri kwa sababu hatuwezi kimkataba kumlazimisha, tulimshauri kwa uwezo wake wa kufanya kazi hana uwezo wa kujenga mradi huu.” 

Profesa Mbarwa, amesema kitendo cha TRC kutia nguvu  kiusimamizi na kitaalamu kumesaidia kuokoa utekelezaji wa mradi wa reli ya kisasa (SGR) kipande cha nne ( Tabora–Isaka,) huku kasi ya ujenzi ikiongezeka na kuimarisha matumaini ya kukamilika kwa wakati mwaka mnamo mwaka 2028.

"Chini ya Mkurugenzi Mkuu wake, Mhandisi Machibya Shiwa, TRC imefanya kazi kubwa kuweka mazingira wezeshi yaliyomuwezesha mkandarasi kuendelea na utekelezaji wa mradi huo, ambao umekuwa ukisuasua na sasa kupitia vyombo mbalimbali vya habari, Watanzania wanashuhudia hali ya mambo katika mradi huo," amesema Prof. Mbarawa.

Amemshukuru  mtendaji mkuu wa TRC Mhandisi Machibya pamoja na timu yote ya uongozi wa TRC na wafanyakazi wote  wa TRC kwa kujitoa na kusimamia miradi hiyo ya SGR.

Akihitimisha, Prof. Mbarawa, ameelezea matumaini yake kwa Shrika la Reli Tanzania, kuhusu ya suala zima la thamani halisi ya fedha inayolipwa kwa ajili ya ujenzi wa miradi hiyo ya SGR inakuwa na thamano halisi ya malipo husika (value for money).

Awali, Mkurugenzi Mkuu wa TRC  Mhandisi Machibya Shiwa alisema TRC inaendelea kusimamia mradi kwa karibu, ikiwemo kuhakikisha upatikanaji wa vifaa muhimu na udhibiti wa matumizi ya fedha ili kuongeza kasi ya utekelezaji.

Kipande chan Tabora–Isaka kina urefu wa kilomita 165 na kina thamani ya dola za Marekani milioni 909.1, ikijumuisha kodi ya ongezeko la thamani (VAT).

Post a Comment

Mpya zaidi Nzee zaidi