-APONGEZA UWEKEZAJI, KUJITEGEMEA KIFEDHA
Mwandishi Wetu,daimatznews@gmail.com
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk. Leonard Akwilapo, ametembelea Banda la Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) akisifia uwekezaji.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk. Leonard Akwilapo, akisaini kitabu cha wageni, kathka Banda la NHC, viwanja vya Sabasaba Dar es Salaam Julai 5, 2026.
i na kujitegemea kwa shirika hilo.anayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere.
Katika ziara hiyo, Waziri Akwilapo alipokelewa na Mkuu wa Kitengo cha Habari wa NHC, Yahya Charahani, pamoja na timu ya shirika hilo Sabasaba, ambapo pia alipata maelezo mbalimbali kuhusu shuguli za shirika hilo na kujionea miradi mbalimbali ya makazi, biashara na matumizi mchanganyiko.
Miradi hiyo inatekelezwa maeneo mbalimbali nchini, pamoja na fursa za uwekezaji zinazotolewa na Shirika la Nyumba la Taifa.
Baada ya kupatiwa maelezo ya kina kuhusu maendeleo ya miradi hiyo, Dk. Akwilapo ameeleza kufurahishwa na kiwango kikubwa cha uwekezaji kinachofanywa na NHC, akisema kimefungua fursa nyingi za makazi, biashara, ajira na kuchochea ukuaji wa uchumi wa Taifa.
"Mmefanya kazi kubwa sana. Miradi hii inaonesha uwezo mkubwa wa NHC katika kuendesha uwekezaji wenye tija na kuleta manufaa kwa Watanzania," amesema Dk Akwilapo.
Amelipongeza shirika hilo kwa kuendelea kujiendesha kwa ufanisi wa kibiashara, akibainisha kuwa NHC ni miongoni mwa taasisi za umma zinazofanya vizuri na kujiendesha kwa nguvu zake, bila kutegemea ruzuku ya Serikali tofauti na baadhi ya taasisi zilizoshindwa kuhimili ushindani na kupoteza nafasi yake katika uchumi wa Taifa.
"Miradi yote mnajitegemea wenyewe, hamtegemei tena Serikali. Hiki ni kitu kikubwa sana. Hongereni sana kwa mafanikio hayo," amesisitiza Dk.Akwilapo.
Ameitaka NHC kuendelea kusimamia kikamilifu ukusanyaji wa mapato na madeni yake kwa kuzingatia sheria na taratibu, akisisitiza kuwa hakuna mdaiwa anayepaswa kupewa upendeleo.
"Msitishike linapokuja suala la kudai malipo yenu halali. Hakuna mdaiwa anayepaswa kuogopwa. Wote wapeni ankara zao za madeni kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizopo," amesema.
Dk. Akwilapo amebainisha kwamba uwekezaji mkubwa unaofanywa na NHC umeendelea kuongeza upatikanaji wa makazi bora, fursa za biashara, ajira na uwekezaji, ambapo ameliagiza shirika hilo kuendelea na kasi hiyo ya ubunifu na utekelezaji kwa manufaa ya Watanzania.
Katika tukio hilo Mkuu wa Kitengo cha Habari wa NHC, Yahya Charahani amesema Shirika Nyumba la Taifa linaendelea kuwakaribisha wananchi kutembelea banda lake, lililopo Mtaa wa Biashara ndani ya Viwanja vya Sabasaba ili kupata taarifa kuhusu miradi ya makazi, biashara, upangishaji, ununuzi wa nyumba na fursa mbalimbali za uwekezaji ilizonazo akianikiza kauli mbiu ya shirika; "Karibu NHC Sabasaba – Tujenge Taifa Letu Pamoja."

Chapisha Maoni