WAZIRI DK JAFFARI AITA WANANCHI SABASABA

 Na Hellen Ngoromela

NAIBU Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dk. Jaffari Seif, amewataka wananchi kutembelea banda la Ofisi ya Waziri Mkuu ili kupata huduma nyingi zinazohusu ofisi hiyo kwa wakati mmoja.

Dk. Seif ameeleza hayo Julai 10 alipotembelea banda la ofisi ya Waziri Mkuu katika maonyesho ya Jubilei ya dhahabu ya miaka 50 ya Sabasaba 2026.

Amesema kwa kiasi kikubwa wananchi wenye uhitaji wa masuala mbalimbali ya kiserikali wamekuwa wakitumia muda mwingi kufuata zilipo ofisi lakini maonyesho hayo yamewarahisishia kuzipata viwanjani hapo.

"Nilichofurahishwa na maonyesho haya ni namna yalivyopiga hatua, inapendeza kuona banda moja lina ofisi nyingi

"Wananchi waje kwa wingi kutembelea banda hili ili waweze kupata huduma kwa wakati hapa kuna ofisi za Tamisemi, Tarura(Wakala wa Barabara Nchini) WCF(Mfuko.wa fidia.kwa.wafanyakazi) na nyingine, " amesema Naibu waziri huyo.

Alitumia jukwaa hilo kuwakaribisha pia wazazi na walezi wanaohitaji huduma za kuhamisha watoto shule kutumia fursa ya maonyesho ya Sabasaba kwenda kupata huduma.

Post a Comment

Mpya zaidi Nzee zaidi