Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Januari, 2026

Matokeo Kidato cha nne 2025, haya hapa

Picha
  Mwandishi Wetu Baraza la Mitihani la Taifa(NECTA), limetangaza Matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne wa mwaka 2025, uliofanyika Novemba mwaka jana. Kwa matokeo ya kijana wako, binti yako, jamaa au wewe mwenyewe, fuata kiunganishi hapa chini;    https://matokeo.necta.go.tz/results/2025/csee/results/s4213.htm

Ndoto mabasi ya umeme Z'bar yatimia

Picha
 Ndoto imetimia, ndivyo unavyoweza kueleza, baada ya awamu ya kwanza ya mabasi ya Mradi wa Mabasi Yanayotumia Umeme (Zan Bus) kuwasili katika Bandari ya Malindi, Zanzibar. Kuwasil kwa mabasi hayo ya mradi unaoratibiwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) na utasimamiwa na Kampuni ya Usafirishaji ya Unitrans kutoka Afrika Kusini ni kutimia kwa ndoto ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), kupunguza taabu ya usafiri kwa wananchi. Mabasi hayo 10 yamawasili Januari 26, 2026  na kuelekea katika maegesho ya Stendi Mpya ya Kijangwani, Mkoa wa Mjini Magharibi  yakitarajiwa kuanza kutoa huduma rasmi za usafiri wa abiria mwezi ujao Februari. Hatua hiyo pia inalenga kupunguza msongamano wa magari barabarani pamoja na kuboresha usafiri rafiki wa mazingira Zanzibar. Mradi huo wa Zan Bus unaotarajiwa kuendelea kutekelezwa hatua kwa hatua  ni sehemu ya juhudi za Serikali ya Awamu ya Nane ya uongozi wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dk. Hussein ...

NHC yaendelea kugusa maisha ya jamii: Wajasiriamali Kinondoni wapapatiwa mashine za uzalishaji

Picha
Mwandishi Wetu, daimatznews@gmail.com Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) limeendelea kudhihirisha kwa vitendo dhamira yake ya kuchangia maendeleo ya jamii kwa kukabidhi mashine ya kisasa ya kukamulia juisi kwa vikundi vya wajasiriamali wasioona katika wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam—hatua inayolenga kuwawezesha wananchi kiuchumi na kuongeza thamani ya shughuli zao za uzalishaji. Watumishi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), wakishusha mashine ya kutengenezea juisi ya miwa kisha kuikabidhi kwa kikundi cha wajasiriamali wenye ulemavu wa macho Kinondoni, Dar es Salaam. Mashine hiyo imetolewa na NHC kuwasaidia wajasiriamali hao waweze kujikimu kimaisha. Akizungumza kwa niaba ya vikundi hivyo, Katibu Mkuu wa Chama cha Wasioona Kinondoni, Vitalis Mdoe, ameishukuru NHC kwa kuitikia ombi lao na kutoa msaada huo muhimu, akisema mashine hiyo itasaidia kwa kiasi kikubwa vikundi vinavyojihusisha na utengenezaji wa juisi kuongeza uzalishaji, ubora wa bidhaa na hatimaye kipato. "Tumesh...

NHC YAFIKISHA BUNGENI DIRA YA MAGEUZI, TEKNOLOJIA YA MAKAZI BORA

Picha
  - Utafiti na nyumba nafuu zatajwa suluhisho la baadaye - Kamati ya Bunge yataka utafiti kwa vifaa, teknolojia za kisasa kupunguza gharama za ujenzi - Enzi za Mwalimu Nyerere hadi Dira ya 2050, NHC yathibitisha uwezo wa taasisi za umma kujitegemea na kuleta tija. Mwandishi Wetu, daimatznews@gmail.com Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), limeweka wazi mkakati wake wa muda mfupi, wa kati na mrefu wa kuboresha upatikanaji wa makazi bora na ya gharama nafuu nchini mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, likisisitiza matumizi ya teknolojia za kisasa za ujenzi, utafiti wa kina wa vifaa mbadala pamoja na uendeshaji wa miradi kwa ufanisi wa kibiashara, unaolinda dhamira ya kijamii. Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Hamad Abdallah, amebainisha hatua hizo wakati akiwasilisha taarifa ya Shirika hilo mbele ya Kamati ya Bunge, Januari 15, 2026 ambapo ameeleza kuwa NHC imejipanga kikamilifu kuendana na mahitaji ya sasa na ya baadaye ya Watanzania, kufuatana na Dira ya Taifa...

MBUNGE AFARIKI DUNIA, KUZIKWA LEO DAR

Picha
Mwandishi Wetu, daimatznews@gmail.com Mbunge wa Viti Maalum,Halima Idd Nassar amefariki dunia leo Jumapili Januari 18,2026 katika Hospitali ya Moyo ya Jakaya  Kikwete (JKCI), alipokuwa akipatiwa matibabu.  Marehemu Halima Idd Nassar Taarifa ya Bunge imemnukuu Spika wa Bunge, Mussa Azzan Zungu akitangaza kifo hicho na kutoa pole kwa familia ya marehemu, wabunge, ndugu, jamaa na marafiki. Taarifa hiyo, imeeleza kuwa Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na familia, inaratibu mipango ya mazishi. Katika hatua nyingine, Ofisi ya Bunge imetoa tangazo linaloeleza kuwa marehemu Halima Idd Nassar atazikwa leo  saa 10 jioni katika makaburi ya Kibada kwa Dole Kigamboni, jijini Dar es Salaam. Marehemu Halima, aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum akiwakilisha wafanyakazi, alikuwa mkazi wa Kigamboni, alizaliwa tarehe 12, Machi, mwaka 1980. Taarifa rasmi ya Ofisi ya Bunge soma hapa chini;

SERIKALI YAKAZIA MACHO UJENZI BARABARA ZA HARAKA KWA MPANGO WA PPP

Picha
-Waziri Mkuu awaongoza mawaziri, PPP Center kusonga mbele Mwandishi Wetu, daimatznews@gmail.com Serikali imeongeza kasi ya kutafuta suluhu ya msongamano wa magari katika barabara kuu kwa kukazia macho ujenzi wa Barabara za Haraka kwa mpango wa ubia, hatua itakayoongeza kasi ya huduma za usafiri na usafirishaji hivyo kuchochea ukuaji wa uchumi wa taifa. Waziri Mkuu, Dk. Mwigulu Nchemba akiongoza kikao cha kazi kuhusu ujenzi wa miradi  ya Barabara za Haraka (Express Ways), kupitia mfumo wa Ubia Kati ya Umma na Sekta Binafsi nchini (PPP) mjini Dodoma Januari 17,2026. Katika kusukuma mbele ajenda hiyo, Waziri Mkuu, Dk. Mwigulu Nchemba ameongoza kikao cha kazi kuhusu ujenzi wa miradi hiyo ya Barabara haraka (Express Ways), kupitia mfumo wa Ubia Kati ya Umma na Sekta Binafsi nchini (PPP). Kikao hicho kilichofanyika Januari 17, 2026 kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu, kimewajumuisha pia Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu, William Lukuv...

WAZIRI MKUU, BALOZI WA JAPAN NCHINI WATETA DODOMA

Picha
Waziri Mkuu Dk. Mwigulu Nchemba amekutana na Balozi wa Japan nchini Tanzania Yoichi Mikami na kujadiliana naye kuhusu masuala ya uchumi, miradi ya maendeleo na uwekezaji kati ya nchi hizo. Waziri Mkuu Dk. Mwigulu Nchemba (Kulia) akizungumza na Balozi wa Japan nchini, Yoichi Mikami ofisini kwake jijini Dodoma Januari 14, 2026.  Dk Mwigulu amekutana na balozi huyo Jumatano, Januari 14, 2026, ofisini kwake Mlimwa jijini Dodoma, ambapo ameishukuru Japan kwa kuendelea kushirikiana na Tanzania kukamilisha ujenzi wa miradi mbalimbali kama vile barabara ya Arusha hadi Holili, Bandari ya Kigoma, miradi ya kilimo na upatikanaji wa vifaa tiba vya huduma za afya ya mama na mtoto. “Serikali itahakikisha kuwa miradi hii inatekelezwa kwa ufanisi mkubwa na inakamilishwa kama ilivyopangwa,” amesema Dk. Mwigulu  Dk. Mwigulu ametumia fursa hiyo kutuma salamu za pongezi kwa Waziri Mkuu wa Japan, Bibi Sanae Takaichi kwa kuteuliwa kushika nafasi hiyo tangu Oktoba, 2025 na kuweka historia ya kuwa mw...

MABILIONEA 10 WENYE NGUVU, WA KUFUATILIWA ZAIDI AFRIKA MWAKA 2026

Picha
  Mwandishi Wetu, daimatznews@gmail.com Mwisho wa mwaka 2025, mandhari ya uchumi wa Afrika iliendelea kuundwa na ujasiriamali, uwekezaji wa kimkakati huku kukiwa na msisitizo jumuishi  wa kikanda unaokua. Aliko Dangote Licha ya changamoto za uchumi wa dunia na mabadiliko ya mifumo ya biashara, kundi dogo la mabilionea barani Afrika halishikilii tu misimamo yao bali pia linafafanua upya nafasi ya bara hilo katika uchumi wa dunia. Kundi hilo dogo la mabilionea kwa mujibu wa mitandao maarufu ya Forbes na Bloomberg, linajumuisha watu wafuatao barani Afrika mwaka huu wakiwa ndio magwiji katika biashara na ambao ushawishi wao unavuka mipaka ya sekta zao. 1. Aliko Dangote – akiwa na utajiri wa Dola bilioni 23.9 Anaendelea kutawala kama mtu tajiri zaidi barani Afrika, mfanyabiashara huyo wa Nigeria ameunda himaya yenye mchanganyiko wa shughuli chini ya Dangote Group, likijumuisha saruji, sukari na usindikaji wa vyakula. Himaya kubwa ya milionea huyo ni Kiwanda cha Kusafisha Maf...

ZIARA YA WAZIRI DK. AKWILAPO NHC, TASWIRA CHANYA YA MAKAZI BORA

Picha
Katika hotuba yake kwa menejimenti na watumishi wa NHC, Dk. Akwilapo ametoa maelekezo ya wazi na yenye mwelekeo wa muda mrefu, akisisitiza umuhimu wa utafiti wa kina katika kubuni na kutekeleza miradi ya makazi. Ameielekeza NHC kufanya tafiti zitakazowezesha ujenzi wa nyumba bora na za gharama nafuu, hususan kwa wananchi wa kipato cha chini na cha kawaida.  Kwa msisitizo, Waziri ameeleza kuwa unafuu wa gharama, lazima ueleweke kwa kuzingatia makundi tofauti ya Watanzania, hali zao za kiuchumi na mahitaji yao halisi. Maelekezo hayo yameenda sambamba na wito wa kutumia teknolojia za kisasa na bunifu katika sekta ya ujenzi.  

Mambo mapya NHC 2026 ikibeba matumaini mpya ya makazi bora nafuu kwa Watanzania

Picha
  - Ziara ya Waziri Dk. Akwilapo yakoleza kasi - Naibu Waziri ataka watumishi NHC kuwa mfano kwa kumiliki nyumba   Mwandishi Wetu, daimatzanews@gmail.com Mwaka mpya, mambo mapya. Ndivyo unavyoweza kusema kwa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kipindi hiki dunia inapoanza mwaka mpya wa 2026. Mambo hayo mapya kwa NHC yanabeba matumaini mapya ya makazi bora, nafuu kwa Watanzania yakibebwa na shirika hilo huku likijipanga kuongeza zaidi kazi ya utekelezaji miradi yake na tafiti ili kubuni na kupata matokeo chanya katika kutimiza majukumu yake kuwapatia wananchi nyumba bora. Hayo yanabainika wakati wa ziara ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk. Leonard Akwilapo, pamoja na Naibu wake Kaspar Mmuya, katika Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Januari 5, 2026, siku tano tu, baada ya kuanza mwaka mpya 2026. Ziara hiyo iliyoandika historia imekuwa tukio lenye uzito mkubwa katika mwelekeo wa sekta ya makazi nchini. Hii ni kutokana na ukweli kwamba ni ya kwanza kwa ...

Rais Samia 'atembea' katika maneno yake afanya mabadiliko Baraza la Mawaziri

Picha
 -Amtema Simbachawene - Makonda Waziri kamili wa habari Mwandishi Wetu, daimatznews@gmail.com Rais Samia Suluhu Hassan, amelitikisa baraza lake la mawaziri kwa kufanya mabadiliko makubwa, akitengua uteuzi wa Waziri wa Mambo ya Ndani, George Simachawene, huku akimhamisha naibu waziri wa wizara hiyo Denis Lazaro Londo kwenda  kushika wadhifa kama huo Wizara ya Viwanda na Biashara. Rais Samia Suluhu Hassan Taarifa ya Ikulu ya leo Januari 8, 2026, imeeleza kuwa Rais Dk. Samia amemteua Patrobas Katambi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, kutoka kuwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, ambapo Mbunge wa Chaani Zanzibar, Ayoub Mohamed Mahmoud aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Kaskazini na Kusini Unguja, ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani.  George Simbachawene Mabadiliko hayo ya Baraza la Mawaziri yamemgusa Profesa Palamagamba Kabudi aliyeiongoza Wizara ya Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo, ambaye amehamishiwa Ofisi ya Rais Ikulu (Kazi Maalum) huku akimpandi...

Dk. Akwilapo aagiza NHC ifanye tafiti kupata suluhisho nyumba bora za gharama nafuu

Picha
  -Asema usimamizi wa ujenzi ni pasua kichwa kwa wananchi - NHC inaweza kuwaondolea wananchi tabu hiyo - Ataka watendaji wasiwe maafisa mchakato Mwandishi Wetu, daimatznews@gmail.com Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk. Leonard Akwilapo ameliagiza Shirika la Nyumba la Taifa, (NHC), kufanya tafiti na kuja na jawabu la upatikanaji wa nyumba bora nafuu za kisasa kwa watanzania wenye kipato cha kawaida. Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk. Leonard Akwilapo akisisitiza jambo wakati akizungumza na wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa, (NHC),jijini Dar es Salaam leo, Jumtatu Januari 5, 2026. Dk. Akwilapo ametoa agizo hilo leo Januari 5, 2026 Makao Makuu ya Shirika hilo jijini Dar es Salam, alipofanya ziara yake ya kwanza kujitambulisha katika shirika hilo pekee, lililo chini ya wizara yake, tangu alipoteuliwa kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. “Fanyeni tafiti za nyumba za gharama nafuu kwa watanzania wa kawaida. Nawatuma mje...