NHC na safari ya miaka 64 ya Uhuru, miaka 63 ya kujenga makazi bora
- Ni shirika lililoanzishwa na Mwalimu Nyerere linabeba ndoto ya makazi ya kisasa kwa kila Mtanzania
-Miradi ya ubia, fedha, teknolojia vyabeba mwelekeo mpya NHC
Mwandishi Wetu, daimatznews@gmail.com
Tanganyika, sasa Tanzania Bara ilipata Uhuru wake tarehe 9 Desemba 1961.Leo, tarehe 9 Desemba 2025, taifa linatimiza miaka 64 tangu kuanza kwa safari yake ya kujitawala.
Pamoja na ushindi huo wa kihistoria, wakoloni walipoondoka
hawakuacha mpango wowote wa makazi bora kwa Tanganyika huru.
Ni katika mazingira hayo ambapo Serikali ya Tanganyika chini ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, ilitambua kwamba makazi ni hitaji la msingi la binadamu. Mwaka mmoja tu baada ya Uhuru mnamo 1962, Serikali iliunda Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kupitia Sheria ya Bunge Na. 45, ikiwa hatua ya kimkakati ya kuunganisha Uhuru wa kisiasa na ustawi wa jamii.
![]() |
| Baba wa Taifa Mwl Julius K. Nyerere |
NHC mshirika wa safari ya Uhuru
Tangu kuanzishwa kwake, NHC limeendelea kuwa mhimili wa
mageuzi ya sekta ya makazi nchini. Safari ya Uhuru ya Tanganyika imeenda
sambamba na safari ya NHC katika kuhakikisha Watanzania wanapata makazi salama,
bora na ya kisasa.
Shirika hili ambalo leo ni miongoni mwa mashirika makubwa
zaidi ya nyumba barani Afrika, lina mtaji unaokadiriwa kufikia Shilingi
trilioni 5, likitekeleza mageuzi yanayowagusa wananchi, sekta binafsi, taasisi
za fedha na Serikali.
Awamu ya Sita, kielelezo cha matokeo ya mageuzi
Katika kipindi cha Uongozi wa Awamu ya Sita chini ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, ambapo Serikali imeweka msisitizo mpya katika uwekezaji, ujenzi na usimamizi—NHC limeshuhudia ufanisi mkubwa.
![]() |
| Rais Dk. Samia Suluhu Hassan |
Miongoni mwa miradi iliyotekelezwa kati ya 2023/24 hadi
Disemba 2025 ni:
- Jengo la Kitengo cha Moyo, JKCI – Dar es Salaam
- Thamani: Sh bilioni 3.1 – Lilikamilika kwa 100%.
- Majengo ya Ofisi za Wizara 8 katika Mji wa Serikali Mtumba
- Thamani: Sh bilioni 194.
- Jengo la Tanzanite, Mererani – Manyara
- Thamani: Sh bilioni 5.5 – Linaendelea kukamilishwa.
- Jengo la Shule ya Uchumi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
- Thamani: Sh bilioni 9.8.
- Jengo la Makao Makuu ya Ofisi ya Makamu wa Rais – Liko hatua za mwisho, ambalo hivi karibuni Makamu wa Rais, Dk Emmanuel Nchimbi alitembelea na kukagua ujenzi wake.
- Miradi ya Hospitali ya Kanda ya Kusini (Mitengo) na Kanda ya Ziwa (Mwalimu Nyerere).
- Ujenzi wa nyumba 10,000,
- Kuimarisha usimamizi wa miradi ya Serikali,
- Kukuza ubia kati ya sekta binafsi na ya umma,
- Kuunganisha mahitaji ya makazi na kasi ya ukuaji wa idadi ya watu.
- Nyumba 887 za makazi katika Iyumbu, Chamwino, Makete, Chartur na Mlele.
- Nyumba 521 za biashara Mtukula, Medeli, Dar es Salaam na Mwanza.
- Nyumba 1,187 za makazi na biashara Morocco Square na kupitia miradi ya ubia.
- Ununuzi wa nyumba 896, zikiwemo 389 za makazi na 497 za biashara Urafiki, Dar es Salaam.
- Samia Housing Scheme – Awamu ya Kwanza (Kawe)
- Nyumba 560; ujenzi umefikia zaidi ya 85%. Mradi mzima utazalisha nyumba 5,000.
- Kawe
711
- Nyumba 422; umefikia 45%, utakamilika Aprili 2026.
- Golden Premier Residence
- Nyumba 532.
- Kupunguza gharama za ujenzi,
- Kuongeza ufanisi wa miradi,
- Kutoa huduma bora kwa wananchi,
- Kuchangia pato la taifa.
Utekelezaji wa miradi hii si jambo lililotokea kwa bahati.
Ni matokeo ya mageuzi ya kimkakati yaliyoimarisha menejimenti, Bodi na
mwendelezo wa dira ya Taifa katika sekta ya nyumba.
Mpango Mkakati wa NHC: 2015/16–2025
Mpango huu wa miaka 10 uliweka dira ya:
Mpango huu umeonyesha matokeo halisi katika kila mkoa wa
Tanzania.
Miradi Mikubwa Tangu Uhuru
Kwa kipindi cha miaka 63 hadi sasa, NHC imejenga au
kusimamia miradi mikubwa kama:
Na bado kazi inaendelea.
Miradi Inayoendelea
NHC na Sekta ya Fedha
Shirika limeunganisha zaidi ya benki 22, likirahisisha mikopo ya nyumba ya muda mrefu, huku nyumba za NHC zikitumika kama dhamana.
![]() |
| Baadhi ya Watumishi wa NHC wakiwa na watumishi wa Benki ya ABSA, wakati watumishi wa benki hiyo walipotembelea miradi ya NHC Dar es Salaam. |
Sekta Binafsi na Ubia
Serikali ilihuisha Sera ya Ubia mwaka 2022, ambayo leo
imewezesha miradi 20 yenye thamani ya Sh bilioni 191 kuendelea katika maeneo
mbalimbali, ikijumuisha majengo ya kibiashara na makazi.
Safari ya NHC na Zanzibar
Katika kudhihirisha ushirikiano wa Muungano, NHC
lilishiriki kuasisi Zanzibar Housing Corporation (ZHC) mwaka 2014, likitoa
mafunzo na utaalamu, na kubadilishana uzoefu katika Bodi na Menejimenti.
Mbele kuna mwanga
Kwa kutumia wataalamu wa ndani hasa vijana na teknolojia ya kisasa, NHC inaendelea:
![]() |
| Sehemu ya Mradi wa Samia Housing Scheme utakavyoonekana baada ya kukamilika. |
Katika miaka ijayo, NHC limejipanga kuongeza miradi mikubwa
nchini, kupanua ushirikiano wa kimataifa na kutoa ushauri wa kitaalamu katika
taasisi mbalimbali.
Kwa miaka 64 ya Uhuru wa Tanganyika, NHC limebaki kuwa nguzo
thabiti katika safari ya taifa kuelekea makazi bora kwa kila Mtanzania.







Maoni
Chapisha Maoni