Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya afariki dunia Dar
Mwandishi Wetu, daimatznews@gmail.com
Waziri Mkuu na Makamu wa kwanza wa Rais Mstaafu, Cleopa David Msuya,amefariki dunia leo Mei 7, 2025 katika Hospitali ya Mzena, Dar es Salaam.
![]() |
Waziri Mkuu Mstaafu,marehemu Cleopa Msuya |
Taarifa ya kifo cha Msuya,imetangazwa leo na Rais Samia Suluhu Hassan kupitia vyombo vya habari, ambapo ametangaza siku saba za maombolezo kitaifa na bendera zitapepea nusu mlingoti.
Rais Samia amesema marehemu Msuya alikuwa akiugua ugonjwa wa moyo kwa muda mrefu,ambapo amewahi kutibiwa hospitali mbalimbali, ikiwamo Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Mzena alipofariki dunia na nchini Uingereza.
Msuya alikuwa Waziri Mkuu wa Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na alichukua hiyo kutoka kwa mtangulizi wake Edward Moringe Sokoine(Marehemu).
Msuya aliwahi kushika Uwaziri Mkuu mara mbili, mara ya kwanza ikiwa tarehe 7 Novemba, 1980 hadi Februari 24, 1983, huku mara ya pili ikiwa ni kati ya Desemba 5, 1994 hadi Novemba 28, 1995.
Kiongozi huyo pia amewahi kishika pia wadhifa wa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na uwaziri wa fedha.
Hadi kufariki dunia, Msuya alikuwa na nyadhifa mbalimbali za uongozi kwenye taasisi tofauti nchini.
Taarifa zaidi kuhusu
Maoni
Chapisha Maoni