Walivyosubiri moshi mweupe siku ya kwanza
-Ni baada ya kura ya tatu za Conclave
-Asubiriwa Papa wa 267
Mwandishi Wetu, daimatznews@gmail.com
Ilikuwa ni saa 5:50 asubuhi, ambapo moshi mweusi ulipanda kutoka kwenye dohani, (bomba la moshi), juu ya Kanisa la Sistine leo ya Alhamisi Mei 8,2025 ukiashiria kwamba kura ya pili na kura ya tatu za kuchagua Baba Mtaktifu mpya kwa ujumla, hazikutoa mshindi.
Makardinali 133 wanaoshiriki mkutano huo maalum wa kumchagua Papa (Conclave), walipoenda kupata chakula cha mchana, watu waliokusanyika katika uwanja kwa pamoja waliendelea kutazama bomba la moshi kwa matarajio kuona moshi mweupe bila mafanikio.
Kwa mujibu wa Vatican kura zinatarajiwa kuendelea leo majira ya saa 10:00 jioni,huku takriban watu 15,000 wakiwa wamekusanyika kwenye Uwanja wa Mtakatifu Petro wakisubiri tangazo la Papa mpya.
Sarah na Cameron, wanandoa wapya kutoka Indiana wakiwa Rome kwa fungate lao walikuwa sehemu ya umati huo walieleza matumaini yao kuwa Papa mpya anaweza kuwa sauti ya busara katika dunia iliyojaa changamoto.
Kauli hiyo liliungwa mkono na Padre Prashant Padu, mwanafunzi aliyepo jijini Rome kutoka Jimbo Kuu la Bombay, India.
“Kanisa limebarikiwa kuwa na Mapapa wa ajabu,” amesema, akieleza matumaini yake kuwa Papa atakayefuata anaweza kuwaunganisha bora zaidi kati yao wote.
Maoni
Chapisha Maoni